Ads

SABABU YA ONGEZEKO LA IDADI YA MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAELEZWA


Idadi ya mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeongezeka kwa asilimia 39% na kufikia Tsh. 5.3 Bilioni kutoka 3.8 Bilioni, wakati idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 9.1% hadi 869,453 kutoka 9.8 Milioni wiki iliyopita.

Meneja wa Miradi na Masoko DSE, Patrick Mususa amewaambia waandishi wa habari kuwa, kampuni ya bia ya TBL imechangia ongezeko la idadi ya mauzo kwa asilimia 99 kutokana na kaunta zake kupunguza bei ya hisa.

Mususa amesema ukubwa wa mtaji wa soko hilo umepanda kwa asilimia 1% na kufika Trilioni 21.8 kutoka Trilioni 21.6 wiki iliyopita, huku ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umepanda kwa asilimia 0.4% hadi Trilioni 8.19 kutoka Trilioni 8.16 wiki iliyopita.

Hata hivyo, Mususa amezitaja kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni CRDB kwa 51.8%, TBL kwa asilimia 44.44% na DCB kwa 1.22%.

No comments