Ads

UTARATIBU WA KUZIUNGANISHA RASMI RAHCO NA TRL UNAANDALIWA !

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makamae Mnyaa Mbarawa akihutubia mkutano wa kihistoria wa Wafanyakazi wa TRL na Rahco uliofanyika Karakana ya Reli Dar es Salaam Novemba 16, 2016
Imefahamika kuwa uteuzi wa hivi karibuni wa Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Nchini Rahco ni hatua ya makusudi ya awali ambayo imechukuliwa na Serikali kwa lengo la kuziunganisha tena taasisi hizi mbili za reli ambapo kabla ya Oktoba Mosi 2007 zilikuwa Taasisi moja, wakati huo ikifahamika kuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa alianisha msimamo huo wa Serikali wakati akizungumza na Wafanyakazi wa TRL na Rahco katika karakana ya Reli ya Dar es Salaam leo mchana. Tamko hilo lilipokewa kwa furaha kubwa sana na Wafanyakazi zaidi ya 500 waliohudhuria mkutano huo wa kwanza Waziri Mabarawa na Wafanyakazi wa TRL Dar es Salaam tokea ateuliwe kuongoza Wizara.
Alisema hatimaye malumbano na mvutano baina ya TRL na Rahco umefikia tamati sasa msimamo ni kuunganisha nguvu kwa pamoja za wanareli kufanikisha malengo ya kuiletea ufanisi TRL na pia utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa reli mpya ya kisasa (Standard Gauge) nchini kutoka Dar es salaam hadi Mwanza.
Wanareli walitarajia tamko hilo la serikali lingetolewa mapema tokea pale Kampuni ya Rites kutoka India ilipobwaga manyanga kuiendesha TRL Julai 22, 2011 na Serikali kutwaa asilimia 51 za hisa na hivyo kuihodhi TRL kwa asilimia 100 kama inavyoimiliki Rahco.
Tamko la Waziri Profesa Mbarawa limefunga ukurasa wa utata wa uhusiano baina ya TRL na Rahco na kufungua ukurasa mpya wa udugu, maelewano na mshikamano ambao utaleta tija katika kufanikisha malengo ya uendshaji wa huduma ya reli na mapinduzi makubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya sekta hiyo ya usafirishaji husuan ujenzi wa reli mpya na kuimarisha ya zamani ya mita geji ili iendelee kuhudumia kwa ufanisi.

MKUTANO WA PROFESA NA WANARELI KATIKA PICHA:

Mkutano wa Profesa Mbaarawa ulisikilizwa kwa hisia kali!

Wanareli wafuatilia kwa makini hotuba ya Waziri
Mwanareli Shehe Shughuli akichangia katika mkutano wa Profesa Mbarawa
Mwanareli Gwamaka Mwakangale akichangia hoja katika Mkutanao wa Wanareli na Waziri Mbarawa



No comments