Ads

WATANZANIA TUJIDHATITI KUILINDA ATCL ILI IWEZE KUFIKIA MALENGO MAPYA WAKATI ZOEZI LA KUIHUISHA LINAENDELEA!

Na Mwandishi Maalum
Watanzania wote tufahamu ukweli wa msingi kuwa biashara ya usafiri wa ANGA sio sawa na kuuza nyanya ..faida ndio  itakuja lakini sio kazi rahisi. Usafiri wa anga ni huduma ya kimkakati kuwezesha sekta nyingine za kijamii na kiuchumi kufanikiwa ikiwemo hasa utalii! Kama ilivyo sekta ndogo ya usafiri wa reli ni muundo mbinu ya kimkakati ili sekta nyingine zifanikiwe! Kurejesha matrilioni zaidi ya 14 yatakayowezesha kufikisha SGR hadi Mwanza haitokuwa kazi ya mteremko! Mnataka ATCL ishindane na Ethopia Airline ilioanzishwa na Mfalme Haile Selassie mwaka 1945 na kuanza operations 1946 hadi anaondolewa madarakani 1974 ilikuwa sawa na mboni ya macho yake! Hata hawa Teferi Benti na Haile Mariam hawakuigusa! Ni shirika la 4 kwa ukubwa duniani! Mashirika mengine Ethad, Qatar na Emirates ukwasi wa nchi zao umesaidia kupunguza maumivu ya uendeshaji huduma ya ndege zao! Wakati sisi tunashangilia kupokea ndege moja ya dreamliner wenzetu wana oda ya ndege za boeing 777, 787 ..nk zaidi ya 200 emirates oda ilikuwa kuanzia 2015 hadi 2021! Ndio maana sisi kajamba nani haraka sana videge vyetu tungevipata kuanzia 2022 labda hadi 2025! Tumezipata kwa haraka kwa vile tumeenda na cash walalahoi wenzetuinstalments zao zimedoda sisi wa cash tunachukua mzigo! Ndio hata kama uwezo mdogo ndege zetu ni kidogo lazima zizalishe tija naafiki. Faida itakuwa ya ki-corporate zaidi  kusaidia kukua sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii(hasa utalii wafike hapa Tz kama first destination). Mambo mengine ni ubunifu na uwezo wa uongozi kuona fursa ya kushirikiana na Washindani wenza kuitumia mara moja!  Hivi mnajua kuna mi-boeing imepark katika viwanja mbalimbali duniani hasa Marekani ikisubiri Mahujaji kuwasafirisha mwaka mara moja na dharura nyingine? Kuna dharura zikitokea kwa mashirika makubwa sio issue sana! Mathalan Novemba 05, 2015 tukiwa angani kutoka Istanbul kuelekea Toronto kuna abiria alipata dharura ya pumu baada ya kutokuwepo msaada wowote ndani ya ndege! Dege boeing 777 likatua katika wa mji wa Goosebay tukapoteza pale zaidi ya saa! Kwa Turkish Airline haikuwa issue lakini kwa 'ribyonka ATCL' ni issue! Kama Haile Selassie aliikumbatia EA kwa miaka 29 na hata hawa Ma-derg kina Haile Mariam hadi Zenawi waliikumbatia EA zaidi ya miaka 45! Tusianze lugha za kuchoka kabla ya kazi haijaanza! Wenzetu wana destination 125 both passenger na freight services ndio faida ya commitment, uzoefu( miaka 74 sasa),vision, strategy na air business acumen! Ndio kutakuwepo kutumbuana, restructuring nyingi tu mbele ya safari! Ombi langu tu kwa Watanzania na Serikali ni kuwa commited katika KUIATAMIA ATCL NI JUKUMU ENDELEVU! Kama Derg isingeendelea kuiatamia EA pale 1974 haki ya Mungu kwa sasa tungezungumza EA katika kutabaruk kama vile marehemu SABENA na EAA! Wao wameatamia EA sasa kwa miaka 74 sisi kwa nini tushindwe?NAMALIZIA KWA KUSEMA USIONE  VYAELEA VIMEUNDWA!來‍♂  ATCL HOYEE NA JPM HOYEE AENDELEE KUIATAMIA ATCL YETU Watu wabaya wasiinyonge!爐

No comments