Ads

Kamati ya Nidhamu ya Simba yamuhoji Aussems kwa takriban saa moja!




Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba jana Alhamis Novemba 28, 2019 imemuhoji kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems ambaye anakabiliwa na tuhuma mbalimbali

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwanasheria Michael Muhina, ilikutana na Aussems katika kikao kilichoanza saa 11 jioni mpaka saa 12  na nusu

Uongozi wa Simba bado haujaweka wazi kuhusu maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao hicho huenda hapo kesho Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa atazungumza

Kitambi aendelea kusimamia mazoezi

Wakati hatma ya Aussems ikisubiri uamuzi baada ya kikao hicho, kocha msaidizi Denis Kitambi leo ameongoza mazoezi ya kikosi cha Simba kwa siku ya tatu

Kitambi amesema leo wachezaji wameonyesha kuchangamka tofauti na hali ilivyokuwa siku mbili zilizopita

Hata hivyo amesema kukosekana kwa kocha Aussems mazoezini kunawaweka wachezaji katika wakati mgumu.

No comments