Ads

UDOM YAKIRI KUWEPO RUSHWA YA NGONO!


Ijumaa, Novemba 22, 201Dondoo za asubuhi: UDOM yakiri rushwa ya ngono, Lipumba atia neno shahada ya Magufuli na Mkapa aisisimua CUF

Na Mwantumu Saadi wa Opera News:

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na UDOM yakiri rushwa ya ngono, Lipumba atia neno shahada ya Magufuli na Mkapa aisisimua CUF. Kujua kwa kina kuhusu yote hayo, endelea kubaki katika ukurasa huu na usome zaidi.

UDOM YAKIRI RUSHWA YA NGONO

CHUO Kikuu cha Dodoma (Udom) kimekiri mbele ya Rais John Magufuli kuwapo kwa dosari ya baadhi ya wahadhiri wake kuomba rushwa ikiwamo ya ngono kwa wanafunzi.

Kutokana na dosari hiyo, uongozi wa chuo hicho umeunda kamati ya maadili ili kudhibiti unyanyasaji wa kijinsia na kupambana na rushwa ya aina hiyo dhidi ya wanafunzi.

Hayo yalibainishwa jana na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Faustine Bee, katika mahafali ya 10 ya chuo hicho ambayo Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.

LIPUMBA ATIA NENO SHAHADA YA MAGUFULI

Mwenyekiti wa CUF-Taifa Prof. Lipumba amesema ni jambo jema kwa Chuo Kikuu Cha UDOM kumtunuku Shahada ya Heshima Rais Magufuli lakini ameviomba Vyuo Vikuu kuwatazama na watu wa Vyama vya Upinzani wakati wa utoaji wa Shahada hizo za heshima.

“Tuko Wanasiasa tumekuwa kwenye shughuli hizi tumevunjwa mikono na tunaendelea kupambana na Demokrasia na sisi wangetuona kwamba hata Watu wa Upinzani wanastahili kupewa Shahada hizi za Heshima” amesema Lipumba.

MKAPA AISISIMUA CUF

BARAZA Kuu la Uongozi wa Taifa la CUF, limeeleza kuguswa na yaliyomo ndani ya kitabu cha Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa ‘Maisha Yangu, Kusudio Langu.

Akizungumza wakati akiwasilisha maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho jana Novemba 21 Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho Taifa amesema Baraza Kuu limeguswa na yaliyomo ndani ya kitabu hicho ikiwemo uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi pia kusononeshwa na mauaji ya tarehe 26-27 Januari 2001!

Kumalizia dondoo, tuangazie suala la Rais Magufuli kutunukiwa shahada UDOM

Jana Alhamis Novemba 21  Rais wa Tanzania, John Magufuli alitunikiwa shahada ya heshima  ya Udaktari wa Falsafa na Mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Rais Magufuli alifunguka kufuaia hatua hiyo na kusema alipotumiwa barua ya kutunukiwa shahada hiyo ilimchukua mwezi kuijibu kwani alikua akitafakari kwa nini apewe bure bila kuisotea na ilhali yeye hapendi vitu vya dezo na hata baba yake alikuwa hampi kirahisi vitu alivyokuwa akiomba na kutoa mfano kuwa akiomba kalamu alimpa kazi ya kufanya kabla ya kumpatia.

Mbali na hayo, Rais Magufuli amekipongeza Chuo hicho kwa kutambua mchango wake na kuamua kumpatia Shahada hiyo.

Nini maoni yako juu ya hilo mdau wetu, tuandikie kwenye Komenti.

No comments