Ads

King Kaka msanii wa Kenya aliyetoa wimbo tata wa rushwa aomba ulinzi


Msanii wa Rap Nchini Kenya King Kaka

Msanii wa Kenya King Kaka anataka ulinzi baada ya watu wasiojulikana kutoupokea vema wimbo wake mpya unaokemea maovu ikiwemo rushwa.

King Kaka amabye jina lake halisi ni Kennedy Ombina, mwishoni mwa juma alitoa video ya wimbo aliouta ‘Wajinga Nyinyi’, akikosoa maovu miongoni mwa jamii ya Wakenya.

Katika wimbo huo amewatuhumu wazi watu binafsi aliowataja majina moja kwa moja pamoja na wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi uliokithiri huku akiwataka Wakenya kutafakari maovu hayo na kuyarekebisha.

Aliutumia wimbo huo huwatolea wito Wakenya kutafakari ujumbe wa video yake na kuchukua hatua.

Tangu video ya wimbo huo kutoka, imekuwa ndio maarufu zaid mitandaoni nchini Kenya .

Wimbo huo ameuimba kwa mtindo wa ushairi, akitamka maneno kama mtu anayeongea kawaida.

Baada ya kutoa video hiyo aliendelea kutoa dondoo za wimbo wake kwenye mitandao ya mbali mbali ya kijamii ukiwemo wa Twitter, mfano ni ujumbe huu ambapo jeshi la wanamaji la Kenya kwa kuchelewa kumuokoa mama na moto wake waliokufa katika ajali ya gari lililozama majini Mombasa na wabunge wanawake kwa kushindwa kutoa taulo za hedhi kwa wasichana wa shule:

 

Wengi wa Wakenya wanakubaliana na ujumbe wa King Kaka na kusema kuwa alizungumzia matatizo yanayowakumba Wakenya mkiwemo hali ya kiuchumi, huduma za afya na hali ya umaskini ya wakenya wengi.

Baadhi yao ni wakili maarufu na mtetezi wa haki za binadamu nchini Kenya AhmedNasir Abdullahi ambaye anadai alichokisema msanii huyo ni ukweli:

Katika hatua ambayo haikutarajiwa na wengi Mkurugenzi wa bodi ya udhibiti wa maudhui ya filamu (KFCB) aliupongeza wimbo wa tata wa King Kaka.

Dkt Ezekiel Mutua, ambaye amekuwa maarufu kwa kuzifungia nyimbo ‘zinazokiukz maadili’ amewataka pia Wakenya watafakari ujumbe wa msanii anaoutoa katika video hiyo kwa njia ya ushairi.

“Ngoja watu watafakari juu ya ujumbe, lakini ukweli ni kwamba kama msanii wa rap anaweza kuandaa ujumbe kama huo na kutembea -huru ni ushahidi kuwa demokrasia yetu imekomaa. Jaribu hilo Uganda au Rwanda na mambo yatakua tofauti ” Dkt Mutua aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Huku baadhi ya wanasiasa wakisema wimbo huo unawatusi, Dkt Mutua amewataka wale wote wanaohisi kuwa wameathiriwa nao kwenda mahakamani kwani bodi ya KFCB haitaingilia uzalishaji wa wimbo Wajinga Nyinyi.

“Wimbo wa King Kaka wa Wajinga Nyinyi alioutoa ni ushahidi kwamba nchi yetu ni huru. Ametumia kibali cha ubunifu wake kutufanya tufikirie. Yeyote anayehisi amedhalilishwa anaweza kutafuta usaidizi wa kisheria, lakini kama bodi, hatuwezi kuingilia uzalishaji, Mutua anasema.

Wimbo wa King Kaka bado uko kwenye mtandao wa Youtube ukitazamwa na watu zaidi ya milioni moja mpaka sasa

Chanzo BBC swahili

No comments