MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI YATUMIA SHILINGI BILIONI 20.1 UJENZI WA MELI TATU ZIWA NYASA, IMO MELI MPYA YA ABIRIA,MIZIGO
Na Mwaandishi Maalum
Meneja wa Meli za Ziwa Nyasa Abedi Gallus akiwa ndani ya meli mpya ya MV.Mbeya II akionesha viti vya abiria ambavyo tayari vimefungwa wakati meli hiyo ikisubiri kukabidhiwa kwa TPA.
Meneja wa Bandazi za Ziwa Nyasa Abedi Gallus, amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kuna miradi mikubwa minne inayoendelea kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2019/2019 ukiwemo mradi ujenzi wa meli katika Ziwa Nyasa ambao umegharimu Sh.bilioni 20.1 ikiwa ni mkakati wa Serikali kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa ukanda huo.Akizungumza na waandishi wa habari walioko kwenye ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na TPA katika maziwa makuu likiwemo Ziwa Nyasa, Gallus amesema kwa kuzingatia umuhimu wa Ziwa Nyasa katika uendeshaji uchumi wa Taifa letu sambamba na kuwepo kwa changamoto za kiusafirishaji ziwani, Januari mwaka 2015 Serikali kupitia TPA ilisaini mikataba miwili kwa ajili ya ujenzi wa meli tatu, mbili zikiwa za mizigo na moja ikiwa ni ya abiria na mizigo.
Viti na meza vilivyopo eneo la abiria la VIP katika meli mpya ya MV. Mbeya II ambayo tayari ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98 na sasa inasubiri kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA).
Amesema kazi ya ujenzi wa meli mbili za mizigo ulianza mara moja Januari mwaka 2015 baada ya taratibu za manunuzi kukamilika na Mamlaka kuingia mkataba na Kampuni iliyoshinda zabuni ya ujenzi huo.Kampuni iliyotengeneza meli hizo ni Songoro Marine ambayo ni kampuni ya Kitanzania na kwamba gharama za ujenzi wa meli hizo ni shilingi bilioni 20.1.Amefafanua mgawanyo wa fedha hizo kwa kila meli ni kwamba meli ya MV Njombe yenye uwezo wa kubeba tani 1000 kwa wakati mmoja imegharimu Sh.bilioni 5.5, meli ya Ruvuma yenye uwezo wa kubeba tani 1000 kwa wakati mmoja imegharimu Sh.bilioni 5.5 na meli ya abiria na mizigo ya MV Mbeya II yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200 imegharimu Sh.bilioni 9.1.
Meli mpya ya MV. Mbeya II ambayo tayari ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98 na sasa inasubiri kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA).
“Ujenzi wa meli ya MV Ruvuma na MV Njombe ulikamilika Julai mwaka 2017 .Kwa upande wa meli ya abiria na mizigo , ujenzi ulianza Julai mwaka 2017 na kwa sasa umefikia asilimia zaidi ya 98 ambapo tayari watalaam wameshaanza kufanya majaribio ya meli hiyo kabla ya haijakabidhiwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari,”amesema Gallus.Kuhusu manufaa ya mradi wa meli katika kanda ya Ziwa Nyasa ,amesema unalenga kuboresha shughuli za usafirishaji na mzunguko wa kibiashara katika maeneo ya Ziwa Naysa na uwepo wa meli mbili za mizigo na matarajio ya kuingia kwa meli ya abiria kutarahisisha shughuli za usafirishaji katika mwambao huo na hivyo kuboresha hali ya uchumi kwa jamii zinazoishi katika miji ya pembezoni mwa ziwa na kuongeza wigo na muingiliano wa kibiashara.Aidha amesema inatarajiwa kuwa uwepo wa meli hizo za abiria utachangia katika kuongeza shehena ihudumiwayo katika Bandari za Ziwa Nyasa. Uwepo wa mel hizi kutaongeza wigo wa ajira kwa wananchi wa maeneo ya jirani na Ziwa Nyasa.”Wananchi wa Kleya , Mkoa Mbeya , mkoa wa Mbeya , mikoa ya pembezoni mwa Ziwa Nyasa na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla wamepata manufaa kutokana na ujenzi wa meli hizi.Moja ya manufaa waliyoyapata ni ajira mbalimbali katika kipindi chote cha ujenzi wa meli hizi na tunaamini wataendelea kupata ajira katika kipidi chote ambapo meli hizo zitakuwa zikifanya kazi.”
Meli ya MV.Mbeya II ikiwa imeegeshwa katika bandari ya Kiwira iliyopo kwenye Ziwa Nyasa kabla ya kujaribiwa na wataalam .Meli hiyo mpya ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98 na kinachosubiriwa ni kukabidhiwa kwa TPA ili ianze kutoa huduma katika ziwa hilo.
Pia amesema faida nyingine za uwepo wa meli hizo ni kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa katika maeneo ya ukanda wa ziwa hilo kwani ukweli usiopingika usafiri wa majini hasa wa kutumia meli za kisasa ni ni rahisi ukingalinganisha na usafiri kwa njia ya barabara.“Kwa mfano gharama ya kutoa tani moja ya makaa ya mawe kutoka Ruvuma hadi Mbeya ni wastani wa fedha za Tanzania Shilingi 110,000 , gharama hii ni kubwa sana ukulinganisha na gharama za usafirishaji kwa njia ya ziwa Nyasa ambayo ni wastani wa shilingi 85,000.“Pia kuna faida nyingine ya usalama , tunafahamu Ziwa Nyasa ni miongoni mwa maziwa yenye mawimbi makubwa sana hadi kufikia mita 2.5 hali ambayo ni hatari sana kwa wasafiri na mizigo inayosafirishwa ziwani kwa kutumia maboti na ngarawa.Hivyo meli hizi ni salama,”amesema Gallus.
Post a Comment