Ads

Wataalam ufundi vifaa tiba wajengewa uwezo Mloganzila

Na Mwandishi Wetu
    

Mkurugenzi wa HudumazaTibaWizarayaAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatoto, Dkt. Grace Magembeakizungumzawakatiwakufunga mafunzo

Wataalam ufundi vifaa tiba wamepaatiwa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo wakufanya matengenezo ya mashine mabilimbali za kutumika katika utoaji huduma za afya hapa nchini

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika hospital ya taifa ya Muhimbili –Mloganzila , Mkurugenzi wa Huduma za tiba   Wizara ya Afya ,Maendeleo Jamii wazee na watoto Dkt Grace Magembe amewataka wataalam hao kuwajengea uwezo wataalam, wengine ilikuongeza ufanisi kazini

“Hakikisheni mnaacha alama kwa kuwajengea uwezo wataalam wengine ambao hawakupata fursa ya kushirik katika mafunzo haya ilikuongeza idadi ya wataalam wa ufundi vifaa tiba nchini’’ mesema Dkt Magembe

Dkt Magembe amewashukuru Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH)kwa kushirikiana katika kuandaa mafunzo hayo nakueleza kuwa serikali itsendelea kushirikiana nao kwa faida ya pande zote mbili

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila Dkt Julieth Magandi amesema kutolewa kwa mafunzo  hayo kutaendelea kuwapa ujuzi katika kufanya matengenezo ya vifaa tiba kwa wakati ilikuwawezesha watoa huduma za afya kutoa huduma za faya pasipo shida yoyote

Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa mwezi mmoja nakushirikisha wataalam kutoka Dar es Salaam, Dodoma, Tabora, Lindi, Tanga, Geita, Mwanza, Arusha, Pwani, Mtwara, Singida,Mbeya,Kilimanjaro,Shinyanga na Katavi

Baadhiyawataalam wa ufundi vifaa tiba kutoka mikoa mbalimbali nchini wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa ya kijadiliwa wakati wa kufunga mafunzo hayo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. JuliethMagandi akiwapongeza wataalam wa ufundi vifaa tiba waliomaliza mafunzo ya mwezi mmoja hospitalini hapa.Mkurugenzi wa Huduma zaTiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Magembe na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila Dkt. Magandi wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam hao mara baada ya kufunga mafunzo hayo

No comments