KOCHA MKWASA: KATIKA MICHUANO YA VPL MSIMU WA 2019/20 SIMBA INAONGOZWA KWA KUZAWADIWA PENATI!
Shabiki wa Simba akitolewa uwanjani baada ya kupata mstuko Yanga walipofanikiwa kusawazisha mabao mawili waliokuwa wamefungwa na watani zao Simba.
Mo Banka akiisawazishia Yanga kwa kufunga bao la pili wakati wa mtanange wa Watani wa jadi hapo jana katika Uwanja Taifa.
Washabiki wa Simba wakiwa hawaamini kinachotokea uwanjani wakati wa kipindi cha pili hapo jana.
Kocha wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa alikuwa na wakati mgumu baada ya kufungwa mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya watani wao Simba.
Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti dakika ya 43 kabla ya kuongeza la pili dakika za mwanzo(46) za kipindi cha pili.
Yanga ilirudisha mabao yote dani ya dakika 3 za mchezo huo kipindi cha pili kupitia kwa Mapinduzi Balama dakika ya 49. Balama aliachia fataki kali nje ya mita 18 za goli la Simba mkwaju uliomshtukiza Mlinda Mlango Aishi Manula ambaye aliambulia kudaka hewa. Goli la pili lilifungwa kwa mpira wa kuchupia kwa kichwa na mshambuliaji mahiri wa Yanga Mohamed Banka katika dakika ya 52.
Dakika 30 zilizofuatia timu zote mbili zilitandaza kandanda safi huku Yanga wakiionekana kuwashambulia zaidi Simba wakiongozwa na kiungo wao mpya aliyesajiliwa katika dirisha dogo Haruna Hakizimana Niyonzima.
Hadi Mwamuzi wa Kati Jonesia Rukyaa anapuliza kipyenga cha kuhitimisha mtanange huo matokea katika ubao yalisomeka 2:2!
Akizungumza na Waandishi Habari Mkwasa alisema ugumu wa kutopata matokeo dhidi ya Simba ni kutokana na wachezaji wa timu hiyo kuwa wamekuwa pamoja muda mrefu hivyo wanaelewana sana!
Hata hivyo Kocha huyu mwenye uzoefu wa kutosha wa aliwahi kuchezea timu mbalimbali nchini, zikiwemo Yanga na Taifa Stars amesema muda sio mrefu wachezaji wa Yanga watazoeyana na hivyo kutengeneza kikosi mahiri chenye uhakika wa kufanya vizuri zaidi katika VPL na michuano mengine ya kimataifa.
Post a Comment