Ads

MAKAMU WA RAIS ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA SULTAN WA OMAN


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumfariji Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahrouqi alipofika kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Oman Mikocheni Jijini Dar Es alaam leo Januari 16,2020 kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Sultan Qaboos bin Said.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo Katika Ofisi ya Ubalozi wa Oman Mikocheni Jijini Dar Es Salaam leo Januari 16,2020 kufuatia kifo cha Sultan Qaboos bin Said wa Oman.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Wananchi wa Tanzania wameungana na Wananchi wa Oman katika maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mfalme wa Nchi hiyo Marehemu Sultan Qaboos bin Said.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahrouqi alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi huo Mikocheni Jijini Dar es Salaam kwa ajili kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Sultan Qaboos bin said kilikchotokea mwanzoni mwa wiki.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahroqi kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Oman Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo Januari 16,2020 baada ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Sultan Qaboos bin Said.

Akizungumza na Balozi Ali Almahroqi kwa Masikitiko Makamu wa Rais alisema amepokea kwa Mstuko mkubwa taarifa ya kifo cha Sultan Qaboos bin Said aliyefariki tarehe 10 Januari 2020 akiwa na umri wa miaka 79 hivyo Wananchi wote wa Tanzania wanaungana na ndugu zao wa Oman kwenye kuomboleza msiba huo na Mungu ailaze Roho ya Marehemu Sultan Qabbos Mahali Pema Peponi, Amin!

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemtakia kila la heri kiongozi mpya wa Taifa hilo la Oman Sultan Haitham bin Tariq Al Said katika kuwaongoza Wananchi wa Oman.

Nae Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahrouqi amemhakikishia Makamu wa Rais kwamba Nchi yake itaendelea kuimarisha Uhusiano wa Undugu uliokuwepo tokea enzi na enzi.




No comments