Ads

Mane na Oshoala watawadhwa kuwa washindi wa tuzo ya CAF ya wachezaji bora kwa mwaka 2019!




Tuzo za juu za wachezaji bora za Shirikisho la Kandanda Barani Afrika -CAF kwa mwaka 2019 zimewaendea Sadio Mane and Asisat Oshoala, wakati tuzo za Makocha bora zimewaendea Djamel Belmadi na Desiree Ellis. Sherehe hizo ziliambatana na matukio muhimu ya kuendeleza kandanda barani kuanzia siku ya Jumatatu Januari 06, 2020.

Sadio Mane akicheza kufurahia tuzo
Mkongwe Nwanko Kanu wa Nigeria
Mkongwe Samuel Eto'o wa Cameroon
Sherehe hiyo ilioshuhudia kutawadhwa kwa mfalme mpya wa kandanda barani Afrika na Malkia wake ilifanyika katika hoteli ya kifahari na kuhudhuriwa na nyota mashuhuri wa mchezo huo katika kitongoji cha kitalii cha   Hurghada, Misri.

Nyota wa klabu ya  Liverpool na nchi ya  Senegal  Sadio Mane  na Mshambuliaji mwanamama Asisat Oshoala wa Nigeria na Barcelona  wameshinda tuzo hizo za juu Mwanasoka Bora wa kiume na Mwanadoka Bora wa kike kutokana na usakataji kandanda uliotia fora kwa msimu uliopita wa mashindano ya kandanda wa mwaka 2019.
Sadio Mane akishikilia tuzo yake
Jopo la Wachezaji Kandanda wakongwe wa FIFA
Rais wa CAF Ahmad Ahmad akimtangaza Sadio Mane kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka 2019!
Mualjeria Djamel Belmadi alipata tuzo ya Kocha Bora wa mwaka kufuatia ushindi wa nchi yake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa AFCON fainali zilizofanyika nchini Misri Julai, 2019.Tuzo ya Kocha Bora wa Kike kwa mwaka 2019 imetwaliwa na  Desiree Ellis kufuatia kikosi xhake cha Banyanabanya kufanya vizuri katika michuano ya FIFA ya Kombe la Dunia la Wanawake iliyofanyika nchini Ufaransa mwaka jana.

Washindi wa Tuzo za CAF  kwa mwaka 2019 ni pamoja na Mchezaji bora wa Mwaka wa klabu za barani Afrika Youcef Belaïli (Algeria & Esperance / Ahli Jeddah),Mchezaji bora Kijana wa Afrika wa Mwaka: Achraf Hakimi (Morocco & Borussia Dortmund). Aidha timu bora ya Taifa ya Wanawake Barani Afrika ni Cameroon wakati timu bora ya Taifa ya Wanaume Afrika ni Algeria. Hali kadhalika
Mfungaji wa Bora wa Goli wa Mwaka ni Riyad Mahrez (Algeria).
Orodha ya FIFA ya wachezaji  11 bora wa kulipwa wa Mwaka ni pamoja na  Andre Onana; Serge Aurier, Joel Matip, Kalidou Koulibaly, Achraf Hakimi; Idrissa Gana Gueye, Riyad Mahrez. Wengine ni Hakim Ziyech; Mohamed Salah, Pierre Emerick Aubameyang, Sadio Mane.
Pia kocha Bora wa Mwaka Mwanamke Afrika: Desiree Ellis (South Africa)
Kocha Bora wa Mwaka wa Kiume Afria: Djamel Belmadi (Algeria)
Rais Bora wa Klabu wa Mwaka Afrika: Moise Katumbi (TP Mazembe)
Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka Afrika : Asisat Oshoala (Nigeria & Barcelona)
Mchezaji Bora wa Kiume wa Mwaka Afrika : 
Sadio Mane (Senegal & Liverpool).

Sade Mane akiwashukuru wadau kwa kumuwezesha kushinda Tuzo

Zaidi ya Sherehe ya kutoa tuzo kulikuwepo na matukio maalum yaliyofanyika nchini Misri ambapo kulikuwepo na jukwaa maalum kujadili maendeleo ya kandanda barani Afrika. Jopo la wachezaji kandanda wastaafu wakiwemo Youri Djorkaeff, Mido, Clementine Tourena Laura Georges walishiriki zaidi ya majadiliano pia walishiriki kujibu maswali ya Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Cairo. Wachezaji wakongwe kadhaa wanaitambuliwa nacFIFA pia walihudhuria sherehe hizo wakiwemo Samuel Eto'o( Cameroon) na Nwanko Kanu(Nigeria).

Rais wa FIFA Gianni Infantino akisalimiana na Mwanamuziki Nguli wa Tanzania Diamond Platnamuz

Wakati huo huo Mwanamuziki Nguli kutoka Tanzania Diamond Platnumz aliyealikwa kutoa burudani katika sherehe za utoaji tuzo za CAF za 2019, alipata fursa ya kusalimiana na Rais wa FIFA Gianni Infantino. Wengine wanasema kusalimiana huko sio bure Nyota huyo wa Bongo fleva baada ya mafanikio ya kuanzisha kampuni yake ya  Wasafi Media anawiwa kuanzisha na kumiliki Klabu ya Kandanda itakayoendeshwa kwa mfumo wa kisasa.

Diamond na Wanamuziki wake wakitumbuiza..

Akifanya kilichompeleka Misri Diamond alianza show yake katika ukumbi wa Pick Albatros Hugardha  kwa kuwasalimia wageni waalikwa katika sherehe hizo za tuzo za CAF na kuwapagaisha kwa kibao chake matata cha 'Tetema'. Ukweli kibao hicho maarufu na pendwa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla kiliwachangamsha vilivyo Waalikwa wa Tuzo hizo za kila mwaka za CAF.
Diamond wakati akitumbuiza waalikwa wa CAF 2019 GALA .


(Kwa habari zaidi usiache kutembelea Wasafi TV katika Youtube na kusikiliza Wasafi FM)





         


No comments