Ads

BAADHI YA SALAAM ZA TAASISI KUMKUMBUKA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR HAYATI MZEE ABEID AMANI KARUME







































Picha za Hayati Mzee Karume akiwa katika matukio mbalimbali ya kiserikali!









Wakati wa tukio la kuuawa kwa Mzee Karume Aprili 07, 1972 nilikuwa mwanafunzi wa Kidato cha 3 Skuli ya Haile Selassie! Nilifuatilia matukio yote kabla na baada ya kuuawa Mzee Karume hadi narejea Bara Aprili 20, 1974.
Wakati huo sikujua nitakuja kuwa Mwandishi wa Habari!

Naitwa Midladjy Maez,  Aprili 07, 2020 Mtaa wa Ohio, Kivukoni, Ilala, Dar es Salaam.

Najaribu kumkumbuka  Mtangazaji aliyesoma taarifa ya Habari ya  RTD saa 7 mchana Aprili 08, 1972! Siku hiyo kule Unguja tuliamka na mang'amung'amu! Hatukulala vizuri baada ya kutangaziwa curfew jana yake  Aprili 07, 1972 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Aboud Jumbe Mwinyi. Inaelekea kwa makusudi STZ walichelewa kujiunga na RTD! Sasa bomu lililipuka baada ya kumsikia mtangazaji huenda ni 'Mzee wa Maguu 12 ya mtu mzima' Ahmed Jongo akitangaza kwa UKAKAMAVU kabisa! Kwa kumaliza Taarifa ya Habari sikilizeni tena MUHTASARI WAKE:"... MAKAMU WA KWANZA WA RAISI SHEIKH ABEID AMANI KARUME AMEUAWAWA JANA JIONI MJINI UNGUJA  KWA KUPIGWA RISASI.."  ! Sikumbuki kama niliendelea kusikiliza! Baadae David Wakati alitoa tangazo rasmi la Rais wa Muungano kuhusu kuuawa kwa Mzee Karume na kwamba tokea tukio litokee amekuwa akizungumza kwa saa 24 na Baraza la Mapinduzi(BM)!  Chini ya kapeti Mwalimu aliwataka kina Jumbe watangaze kuuawa kwa Mzee Karume alitoa saa 24! Baadae mwafaka ukafikiwa kuwa Rais wa Muungano atangaze. Pia baadae ilipitokea fursa Jumbe alifafanua BM walichelewa kutangaza ili kuwatia kiwewe waliopanga njama za kumuua Mzee Karume kuwa huenda hawakufanikiwa na yuko hai! Bado turejee ni Ahmed Jongo aliyesoma taarifa ya Aprili 08, 1972? Mtangazaji mkongwe Abdallah Idrissa Majura ametatua hicho kitendawili kuwa Msomaji wa taarifa  Habari  hiyo ya kihistoria ni Hayati Godfrey Mngodo aliyekuwa Mtangazaji mmojawapo nguli wa RTD .

Shukran Abdallah Majura Mzee wa Kipusa!


No comments