Ads

HATIMAYE MAWASILIANO YA USAFIRI WA ANGA BAINA YA KENYA NA TANZANIA YARAJESHWA!


Na Mwandishi Maalum-Dar es Salaam



Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliotolewa leo Septemba 16, 2020 jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga nchini-TCAA  Nd. Hamza Johari, ameainisha kurejeshwa kwa huduma za usafiri wa ndege kwa nchi jirani,  unatokana na Waraka wa Serikali ya Kenya uliotolewa jana Septemba 15, 2029 ulioindoa Tanzania katika nchi zilizokuwa zinatakiwa raia wake kuwekwa karantini kwa siku 14 wakiwasili nchini humo.

Taarifa ya Johari imetangaza kuondoa zuio la kutua nchini Tanzania kwa ndege zote kutoka Kenya zikiwemo za mashirika ya Kenya Airways na Fly 540 limited.
Mzozo huo ulianza miezi miwili iliyopita baada ya mamlaka ya Kenya kuchukua hatua hasi kwa kuitenga Tanzania kwa kuwataka raia wake/wasafiri wakiingia Kenya lazima wawekwe karantini ya siku 14(kwa gharama zao) kuchunguzwa maambukizi ya kirusi cha Covid-19. Uamuzi huo ulikuwa unazuia safari za Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kwenda Kenya.
Taarifa ya leo inaruhusu ndege zote za Kenya kutua Tanzania kuanzia leo.


No comments