VIJANA 1539, WAHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI ARUMERU
Na Mwandishi Maalum - Arumeru
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro akitoa hotuba ya kufunga mafunzo ya kijeshi ya Wahitimu 1539 katika Kikosi cha 833 KJ Oljoro jana.
Vijana 1539 Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa, Operesheni Uchumi wa Kati katika kikosi cha 833 KJ, Oljoro Arumeru, Mkoani Arusha.
Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amewataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyoyapata katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii ikiwemo kudumisha amani na usalama kwenye maeneo yao na ujenzi wa Taifa Kwa ujumla.
Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele akiwasilisha salaam za Mkuu wa JKT.
Kaimu Kamanda wa Kikosi Luteni Kanali J.P. Meidimi akisoma taarifa ya mafunzo ya Wahitimu.
Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya amewataka wahitimu hao, kutumia haki yao ya kikatiba kwenda kushiriki na kupiga kura katika Uchaguzi huu ifikapo Oktoba 28, 2020, huku akihimiza kuwachagua viongozi ambao wamefanya kazi kubwa yakuleta Maendeleo Kwa taifa letu ikiwemo kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati, kama iliyokuwa jina la Operesheni yao (Operesheni Uchumi wa Kati - 2020)
Mafunzo hayo, yalihusisha uhodari, uzalendo, umoja na uzalishaji mali.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro akisalimiana Makamanda wa Kikosi cha Oljoro mara alipowasili kikosini.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akikaribishwa rasmi kukagua gwaride la Wahitimu.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akikagua gwaride la Wahitimu
Wahitimu walipata fursa ya kuonesha jinsi walivyoiva katika mbinu zote za medani ikiwemo kupita vizuizi hatari na mapigano bila ya matumizi ya silaha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro alipata fursa ya kuwazawadia Wahitimu bora wawili katika ukakamavu na pia mafunzo ya kijeshi kwa ujumla
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro alipata pia fursa ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Ufugaji wa Kuku wa Kikosi .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro katika jukwaa kuu pamoja na Makamanda wakiangalia maonesho ya ukakamavu yaliokuwa yakioneshwa na Wahitimu.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akibadilishana mawazo na baadhi ya Wahitimu.
Mafunzo hayo yalianza tarehe Agosti 03, 2020 na kufungwa jana Septemba 18, 2020 na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro.
Post a Comment