Ads

VIONGOZI WA DINI ARUMERU WAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA MATOKEO MAKUBWA

Na Mwandishi Maalum - Arumeru



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro

Viongozi wa Dini Wilayani Arumeru wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa utendaji wenye matokeo makubwa. Aidha wamemshukuru Mwenzi Mungu kwa kuijalia Tanzania Kiongozi mwenye Maono makubwa kupitia  Rais Dk John  Magufuli.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa hafla fupi ya chakula cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro na Watumishi wa Dini ya Kikristo, ambayo imefanyika wilayani humo hivi karibuni.

Wachungaji na Maaskofu wamepongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa inazozifanya na kuleta Maendeleo makubwa kwa wananchi.


Rais Dk John Magufuli

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mkuu wa wilaya Arumeru, amewashukuru viongozi wa dini kwa namna wanavyozidi kuliombea taifa letu, na kueleza kuwa matokeo ya maombi yao ndio yanayosukuma kasi kubwa ya Maendeleo anayoifanya Mhe. Rais Dr. John Pombe Magufuli. na serikali nzima ya awamu ya tano. Nd Muro alitaja baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Nyerere Mto Rufiji la Ufuaji wa Umeme mkubwa  -JNHPP, Reli ya Kisasa SGR na ufufuaji wa huduma za usafiri wa anga kwa ununuzi wa ndege mpya 11.


Baadhi ya Wachungaji wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd. Jerry Muro


Wakati huo huo Nd Jerry Muro amebainisha fursa mbalimbali ambazo viongozi wa dini wanaweza kuziibua na zikaleta Maendeleo makubwa ya kanisa.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro akishiriki kugawa chakula kwa waalikwa.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro akishiriki kula na wageni wake huku wakibadilishana uzoefu wa fursa za kiuchumi zilizopo wilayani Arumeru.


Mchungaji Musa wa Kanisa la Uti wa Uzima Arumeru ni mmojawapo aliyevutiwa na maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro kuhusu fursa za kiuchumi zilizoelezwa kuwepo Arumeru ambazo Makanisa wanaweza kuzitumia kuongeza ufanisi wa huduma zao kwa jamii!


Mchungaji Vaileth Shayo pia ni mmojawapo aliyevutiwa na maelezo ya fursa yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro.


Askofu Manase Amon wa Kanisa la Kisemwe ni mmojawapo aliyevutiwa na maelezo ya fursa yaliyobainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nd Jerry Muro.

Viongozi wa dini wamemshukuru Mkuu wa Wilaya na Serikali nzima ya Awamu ya Tano, kwa kuendelea kuwapa kipaumbele na kuwashirikisha katika mchango wa Maendeleo ya Taifa.


No comments