WAFANYAKAZI WA CHUO CHA MIPANGO WAASWA KUENDELEA KUJITUMA
Na Mwandishi Maalum- Dodoma
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Prof. Hozen Mayaya ( katikati) akiendesha kikao cha 14 cha Baraza la Wafanyakazi juzi Alhamisi Septemba 17, 2020 katika Ukumbi wa Baraza ulipo chuoni hapo. Kushoto ni Katibu wa Baraza Bibi Stellah Masanja na Kulia ni Katibu Msaidizi Wakili Gulliver Simime
Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini juzi Alhamisi Septemba 17, 2020 limefanya Kikao chake Cha 14 katika Ukumbi wa Baraza Jengo la Pili la Taaluma, Kampasi Kuu Dodoma.
Pamoja na mambo mengine Kikao kilijadili na kupitisha Matumizi ya Mfumo wa Malipo Serikalini ( MUSE); Tathmini ya Utendaji Kazi kwa Wafanyakazi kwa Mwaka 2019/20; na Rasimu ya taratibu za uendeshaji wa Misiba.
Aidha, wakati akifunga kikao Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Prof. Hozen Mayaya amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wote wa Chuo kwa utendaji kazi wao mzuri katika kipindi kilichopita na kuwaasa waendelee na moyo huo huo wakufanya kazi kwa bidii, maarifa, na weledi wa hali ya juu ili kuona malengo ya Chuo na Taifa ya kuzalisha wataalamu bora wa masuala ya mipango ya maendeleo wanaokidhi mahitaji ya soko.
Pichani Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakifuatilia kwa makini majadiliano ya kikaoni
Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Chuo cha Mipango Prof. Mayaya (katikati walio kaa) na Wajumbe wa Baraza. Kulia kwa Mwenyekiti ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) Taifa Dkt. Paul Loisulie na kushoto kwa Mwenyekiti ni Katibu Msaidizi wa RAAWU - Kanda ya Kati Bibi Diana Kweka.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na viongozi wa vyama vya wafanyakazi toka THTU Taifa Dkt. Paul Loisulie na Katibu Msaidizi RAAWU Kanda ya Kati Bibi Diana Kweka kama kanuni ya uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi zinavyotaka.
Post a Comment