KAMPUNI YA RELI
TANZANIA(TRL)
Taarifa kwa Vyombo vya Habari (Press release)
HATIMAYE ABIRIA 540 WA TRENI YA DELUXE WALIOKWAMA STESHENI YA SOGA
MKOANI PWANI WAMESAFIRISHWA KWA MABASI 9
KUJA DAR ES SALAAM LEO JUMATATU NOVEMBA 28, 2016
Abiria
540 wa treni ya Deluxe iliokwama katika stesheni ya Soga mkoani Pwani jana
usiku hatimaye wamesafirishwa kuja Dar es Salaam kwa mabasi 9 yaliyokodiwa na Kampuni ya Reli
Tanzania (TRL). Zoezi lilianza saa 4:05
hadi saa 05:30 leo auibuhi.
Treni
ya hiyo illikwama tokea usiku wa kuamkia leo kufuatia treni ya mizigo iliokuwa
ikienda bara kupata ajali ya mabehewa yake mawili kuacha njia kati ya stesheni
za Pugu na Pugu Mpiji.
Tayari
wakati taarifa hii ikitolewa njia imefunguliwa kwa shughuli za uendeshaji wa reli
ya kati kuendelea.
Imetolewa
na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu
Masanja Kungu Kadogosa
Novemba
28, 2016
Post a Comment