UONGOZI WA TRL WAMEZINDUA HUDUMA MAALUM YA USAFIRISHAJI SHEHENA WA ‘BLOCK TRAIN KWENDA BURUNDI MACHI 31, 2017 KUTOKA MALINDI YARD BANDARINI.
(TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI (PRESS RELEASE)
Imefahamika
kuwa huduma maalum ya usafirishaji
shehena wa treni nzima ‘block train’ imezinduliwa rasmi na Uongozi wa TRL kwenda Burundi katika kituo cha Malindi bandarini Dar es Salaam
Machi 31, 2017.
Huduma ya
block train iliozinduliwa ni maalum kwa wafanyabiashara na kampuni binafsi wenye shehena
kubwa za mizigo kutosheleza mabehewa 20
ambapo hurahisisha kuisafirisha moja kwa moja hadi kwa mpokeaji( mwenye mzigo).
Kwa mujibu
wa taarifa ya Uongozi wa TRL treni hiyo yenye mabehewa 20 imebeba malighafi ya
chuma( iron coils) mzigo unaosafirishwa na Kampuni ya UBUCOM ya Burundi na
utachukua muda wa siku 3 kuwasili Kigoma na siku moja kuwasili mjini Bujumbura.
Burundi.
Aidha
taarifa zaidi zimeainisha kuwa TRL imepunguza gharama za usafirishaji wa mizigo
ya kawaida (loose cargo) na ile iliohifadhiwa katika makasha kwenda Burundi.
Hivi sasa TRL inatoza jumla ya Dola za Kimarekani (USD)3,056 kwa behewa moja la
mizigo ya kawaida na USD 3024/= kwa mizigo iliofungwa katika makasha hadi
Bujumbura Burundi ikilinganishwa na gharama
ya USD 3500/= ikisafirishwa barabarani.
Gharama za
TRL zinahusisha pia uhudumiaji shehena
bandarini Dar es Salaam, Kigoma na
Bujumbura na pia usafiri wa reli hadi Kigoma na wa meli hadi Bujumbura.
Imetolewa
na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TRL,
Nd Shaban
Jumbe Kiko,
Dar es
Salaam,
Machi 31,
2017
Post a Comment