HUDUMA YA TRENI YA PUGU AWAMU ZOTE KUWA NA SAFARI 3 KUANZIA MACHI 27, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) unawatangazia watumiaji wa huduma ya treni ya Jiji iendayo Pugu kuwa kuanzia Jumatatu Machi 27, 2017 ratiba yake ya kawaida ya safari 3 kwa awamu ya asubuhi na alasiri itaanza tena.
Taarifa imeainisha kuwa kazi ya kutandika reli nzito ratili 80 imekamilika kwa asilimia 75 tokea ilipoanza pale Januari 03, mwaka huu wa 2017. Kati ya vituo vya reli vya Dar es salaam na Pugu ni kuna umbali wa kilomita 20.
Safari ya treni kutoka kituo cha Pugu kwenda kituo Kikuu cha Dar es Salaam kwa awamu ya asubuhi ya kwanza itaondoka saa 12 asubuhi juu ya alama ya pili saa 2:10 na ya tatu saa 4:20.
Aidha jioni treni ya kwanza itaondoka Kituo Kikuu cha Dar kwenda Pugu saa 9::55 alasiri, ya pili saa 12:05 magharibi na ya tatu ambayo ni ya mwisho itaondoka saa 2:15 usiku. Atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake.
Uongozi wa TRL unawashukuru sana wateja wake wa Pugu kwa kwa ushirkiano walioutoa katika kipindi chote cha ukarabati wa reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es Salaam na cha Pugu.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Nd. Masanja Kadogosa,
Dar es Salaam,
Post a Comment