Ads

HATIMAYE BUNGE LAPITISHA MSWADA WA SHERIA WA TRC MPYA!

HATIMAYE MSWADA WA SHERIA WA TRC MPYA WAPITISHWA NA BUNGE !

Hayawi hayawi yamekuwa! Tokea pale Julai 22, 2011 Mkodishwaji Rites ilipoamuriwa aondoke, Wadau wa Reli ambao wako makini kuhusu umuhimu wa huduma ya reli nchini waliishauri Serikali kuziunganisha RAHCO na TRL ili kutumia vizuri rasilimali chache za kuendeleza reli! Hatimaye baada ya miaka 6 yametimia lakini kiukweli huu mchakato umefanyika ndani ya miezi 17 tokea pale Rais John Magufuli alipomteua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano!
Tunafahamu mchakato wa kuandaa Sheria ya Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) ya 2017 haukuwa lelemama hasa ukizingatia lile lililoshindikana kufanyika tokea mwaka 2011 na kufanyika ndani ya miaka miwili ya Awamu ya Tano! Kwa Wanareli watapendelea kuona  kipindi cha mpito kitachukua muda mfupi iwezekanavyo!
Wadau wengi  wanahusisha upitishwaji wa Muswada  huu wa TRC na utekelezaji wa mradi adhimu wa Reli ya kisasa ya  Standard Gauge(SGR). Hapa Wanareli tunafurahi kuwa tunaua ndege wawili kwa jiwe moja!
Mswada umeunganisha Rahco na TRL na wakati huo huo SGR inatuletea reli mpya na huduma ya kisasa ambayo itarudisha hadhi ya reli katika kiwango cha enzi ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na zaidi!
Kwetu Wanareli Septemba 13, 2017 ni siku ya kuzaliwa upya Sekta ya Reli Nchini. Kwa tukio hili tunawajibika kuwapongeza Viongozi wetu wakuu na pia waendelee kututafutia Masanja Kadogosa wengi tu ili ' lost glory' ya reli irejee kwa kasi kubwa!
Udumu msimamo adhimu wa kuendeleza reli nchini wa Mhe Rais Dk John Magufuli na Wasaidizi wake Wakuu wa kisekta ! Hongera..Hongera..Hongera sana Viongoz wetu! Ni matumaini yetu Wanareli na Wadau wote wa Usafiri wa Reli nchini tutakuwa pamoja na kuungana na Serikali kukabili changamoto zote wakati wa utekelezaji miradi ya ujenzi wa miundo mbinu na uendeshaji huduma ya reli nchini kote! Shime tutekeleze bila ya kuchoka kauli mbiu ya Awamu ya Tano:'HAPA KAZI TU!
Pichani:' Rais  Dk John Magufuli na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.

No comments