PROFESA IBRAHIM JUMA AAPISHWA KUWA JAJI MKUU WA SITA NCHINI TANZANIA!
Hatimaye leo Rais John Magufuli amemuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa 6 wa Tanzania baada ya kukaimu nafasi hiyo tokea Januari 18, 2017.
Kushuhudia tukio hilo muhimu Ikulu Jijini Dar es Salaam leo asubuhi ni pamoja na Makamu wa Rais Nd Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Nd Kassim Majaliwa , Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamaganda Kabudi, wakijumuika na Majaji wa Mahakama Kuu nchini wakiongozwa na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali.
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othaman walikuwepo kushuhudia tukio la kuapishwa Jaji Mkuu huyo mpya katika hafla hiyo iliyofanyika mapema Ikulu ya Magogoni Dar es Salaam . Habari zaidi katika picha.....

Rais John Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Juma kushika wadhifa wa Jaji Mkuu mpya wa Tanzania Ikulu Dar es Salaam. |
Post a Comment