Ads

MAMIA WAMUAGA MWANDISHI HABARI NGULI!

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe jana aliongoza waombolezaji katika tukio la kumuaga Muhingo Rweyemamu Mwandishi Habari Nguli katika viwanja vya Mnazi Mmoja na katika mazishi yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijiji Dar es Salaam.
Marehemu Rweyemamu alifariki dunia asubuhi ya  Septemba 2, 2017 katika Hospitali ya Agakhan ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa upungufu wa damu mwilini. Waziri Mwakyembe aliungana na waombolezaji wengine kuelezelea hasara kwa tasnia ya uandishi habari kwa kuondokewa na Marehemu ambaye muda wote alithamini taaluma ya Uandishi wa habari japo alitumikia nyadhifa za kiserikali ukiwemo Ukuu wa Wilaya za Handeni, Makete na Morogoro . Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe! Amina.

No comments