Ads

TAARIFA ZA KAMATI ZA BUNGE KUCHUNGUZA MIKATABA YA ALMAS NA TANZANITE YATUMBUA VIGOGO WA SERIKALI!

Taarifa za Tume za Bunge za Almasi na Tanzanite za sababisha Mawaziri wawili wa awamu ya 5 kujiuzulu!
Hatua hiyo imekuwa ya lazima baada ya Rais John Magufuli kuwataka wateule wake wote waliotuhumiwa na taarifa hizo popote walipo katika ngazi za utumishi wa Serikali wakae pembeni kupisha uchunguzi wa vyombo vya dola.

Leo asubuhi Ikulu Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alikabidhi kwa Rais Magufuli taarifa za tume hizo kwa ajili ya utekelezaji. Ambapo katika mambo anuai yaliopendekezwa ni pamoja na kuwajibishwa wale wote waliokuwa katika nafasi za uamuzi na kulinda maslahi ya Taifa kwa kushindwa kufanya hivyo.
Mawaziri waliojiuzulu ni pamoja na Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene  na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani.

Caption: Wa kwanza Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa, Mhe Simbachawene na Mhandisi Ngonyani

No comments