Ads

TAHARUKI YAZUKA DODOMA BAADA YA MWANASIASA MACHACHARI TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI MCHANA!

Taharuki isiokuwa na mfano imetokea makao makuu ya nchi mjini Dodoma baada ya Mwanasiasa Machachari na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi mchana nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.

Wakati taarifa hii ikichapishwa tayari Lissu alishafanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi na mpango ulikuwa unaandaliwa wa kumsafirisha kwa ndege kwenda Nairobi.
Hata hivyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu alisema  Mbunge huyo atahamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua zote zinazostahili kuwatia nguvuni maharamia waliomjeruhi  Mbunge Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Tayari watu kadhaa mashuhuri nchini wamelaani shambulio hilo miongoni mwao ni Rais John Magufuli katika mtandao wa Twita amelaani tukio la kushambuliwa Lissu amemtakia afueni ya haraka na kuagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua zinazostahiki kuwatia mbaroni na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wahukumiwe adhabu inayostahili!

News update: Tayari Lissu yuko jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi baada ya kusafirishwa kwa ndege maalum jana usiku!

No comments