Ads

Usilolijua Usiku wa kiza

MANENO KUNTU
🏮🍀
Palikuwa na mchoraji mmoja ktk moja ya mji mchoraji huyo alikuwa mwenye umri wa utu uzima.

Alikuwa akichora picha nzuri sana na akiziuza kwa gharama kubwa sana.

Siku moja wakamjia maskini na mafukara wa ktk mji ule wakamwambia.

"Ewe ndugu, unatengeneza kipato kikubwa sana kwa kazi yako hii, lakini kwa nn hutaki kutusaidia sisi watu wa hali ya chini,,,,,

Watazame wenzako wanaouza nyama, ijapokuwa hawana kipato kikubwa lkn kila siku hutoa vipande vya nyama kuwasaidia wasiojiweza."

*Mchoraji hakuwajibu chochote, ISIPOKUA aliwaangalia maskini wale kwa huzuni, kisha akainama*

Wale mafukara wa mji ule waliondoka wakichukizwa na suala lile la mchoraji.

Ikawa wakitangaziana pale kijijini kuwa mchoraji yule m/mungu amemjaalia kipato lkn ni mbahiri si mwenye kuwasaidia wasiojiweza.

🍀Baada ya muda mchoraji yule alianza kuugua lkn hakuna mwanakijiji yeyote aliye kwenda kumuona mpaka akafa.

🍀Baada ya kufa yule mchoraji siku zilipita, lakini cha ajabu wale wauza nyama wakawa hawagawi tena nyama kwa masikini

Wale wanakijiji ikabidi wawaulize wale wauza nyama
Ni kwa nn hawawasaidii tena nyama kama zamani.?

🍀Wauza nyama wakawajibu kuwa mchoraji alikuwa akiwapa pesa kila mwezi kwa niaba ya kuwanunulia nyama wasiojiweza.

Na wawape bure kila siku lkn alipofariki likasimama jambo hilo kwani hazikutoka tena pesa za kuwanunulia wao nyama kwa kuwa mchoraji ameshakufa........

Baadhi ya watu huwenda wakawa wanakudhania vibaya lkn na wengine huenda wakakuona msafi kama maji yasiyoharibiwa.

Tambua hawakuzidishii kitu kwa wao kukuona ww kuwa ni msafi

Na wala hawakupunguzii kitu kwa wao kukudhania vibaya.

Kilichomuhimu ni vile akujuavyo mola wako kuwa ww ni mtu wa aina gani kwani yy ndiye anaejua ya siri na ya dhahiri.

Usimuhukumu mtu yeyote kwa muonekano wake wa nje kwani hujui undani wake.

Kwani hujui undani wake kuna baadhi ya matendo ayafanyayo lau kama ungeliyajua ungemuhishimu sana.

Nakutakia siku njema.

No comments