Ads

HATIMAYE UKARABATI WA DARAJA KATI YA VITUO VYA MOROGORO NA MAZIMBU UMEKAMILIKA !

HATIMAYE UKARABATI WA DARAJA KATI YA VITUO VYA MOROGORO NA MAZIMBU UMEKAMILIKA NA NJIA IMEFUNGULIWA RASMI!

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji wa TRL Nd Focus Sahani alioitoa kwa Waandishi wa Habari amesema kazi hiyo imefanyika usiku na mchana kuanzia Septemba 19, 2017 na imekamilika kabla ya saa 7 mchana leo kama ilivyokadiriwa awali!
Tayari treni ya abiria kutoka bara imepita katika daraja baada ya awali kupitishwa treni nyepesi ya ufundi ambayo ilipita bila ya mushkeli wowote.
Ukarabati huo ulisimamiwa na Kaimu Mhandisi Mkuu Ujenzi Mhandisi Nelson Ntejo...habari zaidi katika picha...

No comments