Ads

ZIMBABWE BILA YA MUGABE ITAKUAJE?


Ya  Robert Gabriel Mugabe yamenikumbusha masahibu ya nchi kadhaa China baada ya Mao, Zaire aka DRC, Cote de Voire, Tunisia, Cameroon ...lakini Zimbabwe inatuhusu! Aprili 18, 1980 Mwalimu J K Nyerere kama Mwenyekiti wa Nchi za Mstari wa Ukombozi Kusini mwa Afrika alitupumzisha Watanzania siku hiyo tujumuike na Wazimbabwe kusherehekea Uhuru wao!
Kuna nchi za Afrika zilizopata bahati ya mtende kwa Marais kung'atuka kwa hiyari: Senegal, Tanzania na Afrika Kusini! Zambia Kaunda alipigwa TKO na Chiluba na kamweka kizuizini kama na yeye alivyoshughulikiwa na Mwanawasa..., Cote de Ivoire mizengwe baada ya kufariki Rais wa kwanza Felix Houphouet -Boigny madarakani ikawa patashika.. Cameroon haiko salama Paul Biya alifanya palace coup kwa msaada wa Ufaransa! Kenya Mzee Kenyatta alipofariki Mombasa Moi aliapishwa kwa mbinde! Na aliendelea madarakani kwa ubunifu mkubwa kama vile Ibrahim Babangida alivyokuwa akiitwa Maradona Nigeria na Moi hivyohivyo Kenya! Afrika Kusini Madiba alifanya maajabu kung'atuka baada ya miaka 4 tu madarakani! China baada ya Mao lilizuka Gang of Four likiongozwa na mjane wa Mao 1976-79 na Profesa Deng Xiaoping aliyehukumiwa kusafisha mabanda ya mifugo enzi za Mao akaanzisha haya mageuzi ya Modenaizesheni ya China kuanzia 1979 na sasa China imebadilika hadi Marekani wanatetemeka kiuchumi! Sisi Tanzania ni nyota sasa kwa madiliko ya kisiasa Mola atujaalie hivi hivi shetani atupitie mbali! Amina! Swali itachukua muda gani Zimbabwe kupata uongozi imara wenye dira! Itachukua miaka mingapi miwili au mitano? Kwa kawaida nafikiri itachukua takriban miaka kati ya 5 hadi 10 labda wabahatike kumpata 'Magufuli' wao mapema ndio kipindi cha mabadiliko kitakuwa kifupi! Kwa wakati huu tete tuwaombee sana Ndugu zetu wa Zimbabwe waelewani katika kipindi kifupi iwezekanavyo! Mungu Ibariki Zimbabwe, Mungu Ibariki Afrika!

No comments