Ads

JPM ATEUA VIONGOZI WA TRC MPYA! KONDORO MWENYEKITI KADOGOSA MKURUGENZI MKUU!


  • Sheria Mpya ya TRC  Na. 10 , 2017 yakabidhiwa kwa Viongozi Wakuu wa Taasisi hiyo 
  • Prof John Kondoro Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TRC mpya!
  • Mkurugenzi Mkuu Nd. Masanja Kadogosa!
  • Watumishi wote wa TRL na Rahco wahamishiwa TRC!

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa leo Jumamosi Machi 03, 2018, amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Nd Masanja Kungu Kadogosa Sheria mpya ya Shirika la Reli TRC Act na. 10 ya 2017.
Katika sherehe hiyo maalum iliyo fanyika mbele ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dr Leonard Chamuriho na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Prof.John Wajanga Aron Kondoro.Waziri amesema wafanyakazi waliopo TRL na Rahco wanahamia katika Shirika jipya la Reli Tanzania (TRC).
Wakati huo huo katika kikao hicho cha kuzindua Sheria ya TRC ya 2017, Mh. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametangaza kuwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, amewateua rasmi Nd Masanja Kadogosa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC mpya na Profesa John Kondoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRC. Uteuzi huo umefanywa na Rais, kwa mujibu wa TRC Railways Act ya 2017.
Baada ya kikao hicho Waziri na Ujumbe wake pia ulipata fursa ya kutembelea maeneo ya Shauri moyo na kuona kazi ya ujenzi wa nguzo za njia ya reli mpya ambayo kuanzia hapo itapita juu mpaka kuingia stesheni ya Dar es Salaam.






.

No comments