Ads

TRENI YA KWANZA YA ABIRIA KWENDA BARA KUTOKA DAR IMEONDOKA LEO MACHI 02, 2018!

Treni ya kwanza ya abiria imeondoka katika Stesheni Kuu ya Dar es Salaam leo Machi 02, 2018 saa 9:00 Alasiri kuelekea bara ikiwa ni mara ya kwanza tokea safari hizo kusitishwa mnamo Januari 11, 2018 baada ya maeneo kati ya Kilosa na Gulwe kuharibiwa vibaya na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha maeneo hayo. Shughuli za usafirishaji zilihamishiwa kwa  muda mjini Dodoma. Kazi ya ukarabati wa eneo hilo zilifanyika usiku na mchana ambapo zilikamilika mnamo Februari 12, 2018. Hata hivyo  kwa ajili ya kuzingatia masharti ya  usalama wa treni za abiria, ni treni za mizigo ndio zilianza kupita sehemu hiyo na baada ya kuhakikisha kuimarika kwa tuta la reli eneo hilo ruhusa ilitolewa kurejesha tena safari za treni za abiria zilizokuwa zinaanzia Dodoma tokea Januari 16, 2018.

Ratiba ya treni za abiria imerejea kama kawaida kwa siku za Ijumaa, Jumapili, Jumanne na treni ya Deluxe siku ya Alhamis kwenda Kigoma.


No comments