Waandishi wa Habari Wakitanzania wachaguliwa katika Programu ya BMIA FJT!
Watanzania wa taaluma tofauti 46 wakiwemo Waandishi Habari wameanza mafunzo ya miezi 6 kupata weledi wa kuchunguza na kuandika habari za Fedha, Uhasibu na Uchumi !
Mafunzo yalioanza tokea Septemba 13, 2019 kwa matayarisho katika Hoteli ya Serena na baadae mafunzo halisi katika Hoteli ya Hyatt Regency kuanzia Septemba 16 hadi 18, 2019.
Kwa mujibu wa Waratibu ambao ni Bloomberg wakishirikiana na Vyuo Vikuu vya Strathmore( Kampasi ya Nairobi), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mafunzo hayo yamegawiwa katika awamu 6(Study Blocks) Awamu hizo ni(2019) Septemba16-18; Oktoba 22-24; Novemba 18 -21; Desemba 10-12;(2020) Januari 28-30 na Februari 25-27, 2020!
Mafunzo pia yamegawiwa kinadharia na vitendo! Darasani na pia muda wote baina ya awamu hizo Washiriki wa mafunzo watajisomea na kufanya mazoezi maalum wakiwa katika makundi maalum na mazoezi binafsi kwa kila mshiriki! Taarifa zaidi kuhusu Programu hii ya Mafunzo inayofadhiliwa na 'Bloomberg Media Initiative For Africa Financial Journalism Training, ni kwamba tayari ishafanyika katika nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Nigeria na Kenya katika awamu ya 2 zimebahatika nchi za Zambia, Ghana na Tanzania.
Post a Comment