Ads

KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE INAENDELEA..

Anaandika Dr Anthony M. Diallo

Kabla ya kusoma makala hii nikwambie tu. Dr Anthony Mwandu Diallo alikuwa rafiki wa Mwalimu. Na wakati ule mwalimu alivyong’atuka Madarakani 1985 waliendelee kuwa marafiki akiwa Mwenyekiti wa CCM na hata alipoachia kiti cha CCM.

Na msiofahamu Dr Diallo mwaka 1995 alichaguliwa mbunge wa jimbo la Mwanza vijijini, na alipoingia Bungeni alikuwa katika kamati ya Fedha na Uchumi. Dr Diallo akiwa Makamu wa mwenyekiti wa kamati Marehemu Akukweti walifanya ziara kukagua miradi ya serikali na walienda Mwitongo, Butiama kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Baba  wa Taifa mbayo wakati ule mradi ule ulisimamiwa na JKT, na ulikwama kutokana na kukosekana kwa fedha!

Dr Diallo na wajumbe wake walivyorudi bungeni alishinikiza serikali itimize ahadi yake kwa kushika shilingi ya mshahara wa Waziri wa Fedha Prof Mbilinyi. Wizara ilibidi kuipatia JKT fedha kumaliza ujenzi huo. 

Ndugu zangu hebu tufaidi huu uhondo wa hii makala kutoka kwa mtu mstaafu wa awamu mbili kama Waziri na rafiki wa Mwalimu; mtu aliyekuwa  kijana sana wakati huo na mjenga hoja safi sana Bungeni akitumikia jimbo lake ambalo baadae lilijulikana kama Ilemela. Dr Diallo anatumikia Chama cha Mapinduzi kama Mwenyekiti wa Mkoa na amekaa ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kwa takribani miaka 17 sasa:

Tunapofanya kumbukizi kidogo niwakumbushe MAFANIKIO YA MWALIMU NYERERE
By Dr Anthony Diallo
CCM- Mkoa Mwanza!

1. TAZARA (CAPE GAUGE RAILWAY- CGR ya kwanza Afrika Mashariki na kati) aliijenga na Mwenzie Kaunda
2. RELI YA SINGIDA-MANYONI
3. Kiwanda cha Nyuzi Tabora
4. Viwanda 11 vya korosho
5. Viwanda 11 vya nguo
6. Kidatu, Mtera,  Kihansi
7. Meli ...Bahari ya Hindi,  Victoria, Nyasa
8.  Ndege 14 za ATC
9. Vyuo Vikuu... Udsm, Mzumbe,SUA
10. Kuimarisha Mabasi ya Railway
11. Kampuni ya Usafiri jijini ya UDA
12. KAMPUNI YA MABASI YA TANZANIA.. KAMATA
13. mashamba ya Mifugo... Ranchi za taifa..Ruvu, morogoro,  KongwA, N.K.
14. National parks 10
15. Vyuo kuwalipa Wanafunzi fedha za matumizi
16.  Wanafunzi secondary kusafiri bure
17. Elimu ya watu wazima... 95%
18. Bugando Hosp, Kilimanjaro na Hoteli za kiatalii 14,  Muhimbili Hosp Extension, KCMC
19. Vyuo vya Kilimo UYOLE,  NALIENDELE,  ILONGA,  UKILIGURU, 
20. Viwanda vya vifaa vya umeme. Kiwanda cha,  baiskeli,  matairi,  vipuri vya magari, radio (Phillips  na National)na betri.
22. Nyumbu trucks
23. Machine za kuchambua Pamba... Ginneries na viwanda vya kutengeneza vipuri vya ginneries;
24. Elimu bure tangu 1972 hadi 1990... Daftari,  Kalamu,  vitabu bure. Shule ya msingi hadi chuokikuu vikuu bure;
25. Huduma za afya bure
26. Mafanikio katika utamaduni na Michezo... Vikundi vya utamaduni na bendi kila mkoa
27. VYAMA vya ushirika wa mazao
28. Alijenga Umoja.... Hakujenga nyumba....alikopeshwa...; alijengewa na Jeshi
29. Aliheshimiwa duniani kote
30. Aliandika vitabu zaidi ya ishirini
31. Bodi za Mazao... Pamba, tumbaku,  Korosho, kahawa
32. Gapex
33. Tanzania Elimu Supplies
34. Tanzania Publishing House
35. Tafico
36. Chuo cha Uvuvi Mbegani
37. Vyuo vya utalii na wanyama pori
38. Vyuo vya Kilimo,  Tumbi, UYOLE,  n.k.
39. Viwanda vya Kahawa na Mazulia
40. Secretarial colleges...Dar na Tabora
41. SHIRIKA LA TANESCO
42. Bwawa la Mindu
43. Kuimarisha Kiswahili kuwa lugha ya taifa
44. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
45, Muungano wa TANU na Afro Shiraz
46. Mbarali, Dakawa Rice farms
47. Kila kijiji kupewa trekta
48. Kila kijiji kupewa ng'ombe 20 wa kisasa
49. Tanganyika packers... Nyama
50. Kiwanda cha Coca-Cola  Shinyanga
51. Mashamba ya zabibu
52. Dodoma wine
53. Moproco
54. Morogoro  Canvas mill...the largest in Africa
55. Mgololo Paper Mill..   The largest in Africa
56. Kiwanda cha bia
57. Kilimo cha matunda Tanga
58. Chakula Bariadi... Kutengeneza Barafu za majumbani na viwandani
59. Saab scania - kibaha..kuunganisha scania
60. Chuo cha Posta,  chuo cha Kodi,  chuo cha Sukari, 
61. Zana za Kilimo Mbeya
62. Shilingi iliyokuwa na thamani kubwa kukaribiana na dola na pauni.
63. Kiwanda cha Kibuku
64. Kiwanda cha Konyagi
64. MECCO
65. Kiwanda cha sigara
66. Kiwanda cha kuchapa vitabu na magazeti... Kiuta
67. Kampuni ya Fenicha
68. National Housing Corporation
69. STC...  State Transport Corporation
70. Tanzania Tourism Corporation
71. Shihata
72. Shirika LA Posta na simu
73. Tangold

Hadi anastaafu Nyerere aliacha viwanda kama 500 vya umma, na mashirika... Achilia kampuni za watu binafsi...na viwanda vya vyama vya ushirika...na mengine mengi....

Alloyce Nyanda
Mtozi

No comments