Ads

RAIA WA MSUMBIJI WALIOKO TANZANIA WAPIGA KURA UCHAGUZI MKUU WA MSUMBIJI


Raia wa Msumbiji walioko Tanzania waliojiandikisha kushiriki uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wamepiga kura wakiwa nchini na kuchagua Rais wa nchi hiyo uliofanyika leo.

Afisa kutoka Ubalozi wa Msumbiji nchini bi Felismina Salegua amesema wananchi hao wa Msumbiji waliojiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo wanatoka katika mikoa ya Raia hao wamepiga kura katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Lindi, Mtwara, Ruvuma na Zanzibar.

Bi Seligua amesema jumla ya wananchi  20,820 walikuwa wamejiandikisha kwa Tanzania Bara kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.

Bi. Seligua alikuwa akizungumza na ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliotembelea vituo vya kupigia kura katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara .

Ujumbe huo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mhe. Salum Rehani wametembelea vituo vya kupigia kura katika wilaya za Namtumbo, Tunduru na Mtwara ili kujionea upigaji kura unavyoendelea.

Awali akikagua maandalizi ya upigaji kura huo Mhe.Rehani aliwahakikisha mazingira ya Ulinzi na usalama ili uchaguzi wao ufanyike kwa ufanisi hapa nchini.

Msumbiji imeendesha zoezi Ka kupigia kura kwa nchi mzima kwa kuchagua rais, wabunge na wawakilishi wengine wa wananchi katika kipindi cha Mika mitano Ijayo.

Raia wa Msumbiji walioko nje ya nchi yao walipata nafasi ya kuchagua rais wa nchi hiyo ambaye ataiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo wagombea wanne   Kutoka vyama vya Siasa vya RENAMO, Frelimo na MDM Wameshiriki

No comments