Ads

KUVAA MAVAZI YA HESHIMA KIUTAMADUNI NI WAJIBU WA KIJAMII WAVULANA KWA WASICHANA!

Msichana mmoja alinunua simu aina ya Iphone. Baba yake alipoiona, alimwuliza binti: “Ni kitu gani cha kwanza ulifanya baada ya kuinunua hiyo simu yako?”
Binti alijibu: “ Nilibandika kioo cha kwenye sehemu ya mbele ya simu ili kuzuia isipate michubuko; na pia nilinunua mfuniko wa hiyo Iphone”
Baba alimwuliza: “Kuna mtu yeyote aliyekulazimisha kufanya hivyo?”.
Binti akajibu: “ Hapana”
Baba akamwuliza swali jingine: “Hudhani kwamba kwa kufanya hivyo ni kama vile unawabeza au kuwatusi watengenezaji?”
Binti akajibu: “Hapana baba! Tena wenyewe ndio wanapendekeza kuweka kitu cha kuilinda hiyo Iphone”
Baba aliendelea kumwuliza binti: “Uliifunika kwa kuwa ilikuwa haina viwango na ilikuwa na sura mbaya?”
Binti: “ Kusema kweli niliifunika kwa kuwa sikutaka iharibike na sikutaka pia ishuke thamani yake.”
Baba akaendelea kuuliza: “ Wakati ulipoweka mfuniko juu ya hiyo Iphone mfuniko huo ulipunguza uzuri wake?”
Binti alijibu:”Nadhani mfuniko huo unaipa Iphone yangu muonekano wa ubora zaidi kutokana na ulinzi unaoipa.”
Baba alimwangalia binti yake kwa upendo na kusema: “Unasema hivyo lakini je, kama ningekuambia ufunike mwili wako ambao una thamani zaidi ya Iphone hiyo ungekubali mara moja?”
Binti akakaa kimya.
SOMO:
Uvaaji usio wa heshima na kuacha sehemu ya mwili wako nje unapunguza thamani na heshima yako.
Kila wakati vaa kiheshima.
Tafadhali tuwalinde wasichana wetu wadogo kwa kusambaza ujumbe huu kwa wazazi wenzetu.

No comments