Kivuli cha mbwaga Sumaye katika uchaguzi wa Chadema kanda ya Pwani!
Kwa ufupi
Aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura ya hapana.
Pwani. Aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura ya hapana.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamisi Novemba 28, 2019 mjini Kibaha Mkoa wa Pwani, Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1995 hadi 2005 amepigiwa kura 28 za ndio na 48 za hapana na kura moja imeharibika.
Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Patrick Ole Sosopi ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).
Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo, Sumaye amesema lililofanyika ni demokrasia japo hana uhakika kama kutoa adhabu kwa mtu aliyekuwa anatumia haki yake kufanya demokrasia ni sahihi.
"Nilitamani ningekuwa na mtu wa kumpongeza, kazi yangu ya ofisi imeisha niwashukuru wote walionipa kura na wale ambao hawajanipa kura," amesema Sumaye
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo baadhi ya wajumbe na wanachama waliokuwepo walilipuka kwa shangwe huku wakiimba nyimbo mbalimbali za chama.
Pia Soma
Kampuni ya Jumia yafunga biashara TanzaniaVIDEO: Nancy Sumari: Ni muhimu watoto kutambua haki zaoBibi Cheka afariki dunia
Walipotoka nje ya ukumbi waliendelea kuimba na kusema wagombea msilale bado mapambano.
Asubuhi akifungua mkutano huo, Sumaye aliwataka wagombea watakaoshindwa kuwa kitu kimoja, watakaoshindwa kuvumilia wajitoe.
Post a Comment