Ads

THROW BACK 2016 OF TRC FATE: NINI KIFANYIKE KUIMARISHA HUDUMA YA RELI NCHINI?

Na M.Maez

Mimi niko Reli kwa miaka 19 nikiandika riwaya kuhusu ups and downs za railways itakuwa ukweli kwa asilimia 75-99! Huduma za Reli  ni kama ng'ombe mkubwa anayetoa maziwa ya uzima kwa sekta nyingine za uchumi na kijamii na kuzifanya zikue na kustawi!    Huduma ya reli wakati wa ukoloni ilikuwa na hadhi ya kidola zaidi kuliko hata vyombo vya kidola kama vile jeshi, Polisi! Ukweli ni kwamba wakati huo vitengo vya hotel catering vya reli vilihudumia Ikulu, legco na state banquet ! Kitengo cha Public relations kilitayarisha taarifa rasmi za Serikali kutokea London na Afrika Mashariki  -newsreel kila wiki! Kwa Ufupi hadhi hii ilipungua baada ya nchi 3 Tanganyika,  Uganda na Kenya kupata Uhuru!  Hata hivyo huduma za East African Railways and Harbours Corporation EARC 

zilikuwa bado zinaridhisha!  Mtakumbuka kutoka Mbamba Bay unasafiri na meli hadi Itungi Port Kyela pale basi la EARC linakuchukua hadi Itigi unapanda treni kwenda Kigoma au Mwanza ambako unapanda tena meli kumalizia safari yako!  Kama kunakuwa na mushkeli wa kuunganisha safari husika huduma za catering na hoteli zilikuwepo nchini kote reli ilikuwepo Dar,  Dodoma, Tabora,Tanga , Moshi, Arusha, Musoma,  Mwanza na Kigoma! Kutetereka huduma za reli kuliashiriwa na kuondolewa Kitengo cha bandari miaka ya mwisho ya 60 na kuundwa East African Cargo and Handling Services na baadae Tanzania Harbours Authority na sasa TPA wana hela hata hawajui jinsi ya kuzitumia! Privilege nyengine ya kidola ilikuwa ifikapo Desemba 31 kila mwaka reli hufutiwa Madeni yake yote ambayo mengi yalitokana na utekekezaji wa kinachoitwa kutimiza public obligation!  Pia Serikali iliongeza asilimia 20 ya bajeti iliyopendekezwa! Reli mwaka wake wa  fedha huanza Januari mosi kila mwaka isipokuwa kuanzia 2015/16! Baada ya kuvunjwa EAC 1977 reli ikawa idara ya kawaida ya Serikali hadhi yake sawasawa na Kampuni ya Chibuku madeni yake kuanzia 1977 hayakufutwa hivyo hadi 1997 TRC ikawa liability fikiria hata siku moja Polisi au JWTZ kuwa liabilities na kufikiriwa   kubinafsishwa!  Reli kama mtu ilianza kuvuliwa nguo 1969 bandari ( source ya petty cash yake) ikapelekea kuondoka vitengo vya road transport na hotel and catering 1990-92 na Mwishowe  Marine 1999! Reli imebaki Chuma kitupu lakini ina umri wa miaka zaidi ya 100! Miaka ya 1977 hadi 2002 wafadhili walipojitoa haikuwa miaka ya ustawi kulikuwa na majaribio mengi yakiongozwa na Benki ya Dunia! Zoezi la  ubinafsishaji halikuleta tija iliyotarajiwa! Rites walisema TRL itafanya hasara kwa miaka 5 na labda 2017  ita break even! Wadau wa TRL Rites hisa 51%  na SMT49% baada ya kuburuzana tokea 2008  ukosefu wa mtaji wa kuendesha TRL ndio ikawa sababu kuu na Rites kutaka kutumia vitendea kazi mitumba kwa kukodi toka India na kutelekeza locos za 88 class za TRC! Ikumbukwe sasa kuna mradi wa kutengeneza upya locos 16 ambapo 10 zimekamilika mradi unaondeshwa kwa pamoja na SMH ya Malaysia katika karakana kuu ya vichwa vya treni Morogoro!  

Sawa Serikali imeshawekeza kati ya 2012- 2015 TZS bilioni 350 lakini uwekezaji umekuja wakati TRL inahitaji mambo Makuu matatu: Working capital,  Mpango wa ajira mpya haraka sana na ukarabati wa karibu 600km za njia ya reli inakadiriwa kuhitaji zaidi ya  TZS200 b! Hii miradi inahitaji kufanyika sambasamba! Mwanareli kijana ana miaka 45! Kuna wimbo unaopendeza wa reli ya kisasa Standard gauge au American gauge 1.435m huu ni mradi maalum ambao ukikamilika inakadiriwa utasafirisha zaidi ya tani 17m! Reli ya sasa mita geji ina uwezo wa kusafirisha tani 6m kwa mwaka ni 2002 tuliweza kusafirisha tani 1.45m!  Kuanzia hapo tumeshuka hadi chini ya tani 200,000 2012-13! Ng'ombe huyu wa maziwa kuwa hai mpaka leo ni dhahiri sio wa Kizungu! Lakini bado Serikali inawajibika kuangalia yale ya enzi za Ukoloni yepi inaweza kuyafanya mojawapo ni kuchukua madeni ya TRL kuanzia 2007 hadi 2015! Hivi sasa vyombo vya fedha collateral ni vitendea kazi vipya vikiwemo vichwa vya treni 21 lakini bado wanahitaji tuwe na uendeshaji unaojiweza! Sifahamu Serikali za awamu ya 3 na 4 zimetumia trilioni ngapi kujenga mtandao wa barabara za kisasa nchini lakini kuchelewa kuwekeza ipasavyo katika reli uhai wa hizo  barabara   ni mfupi sana ni sawa na kuzitumbukiza hizo trilioni baharini! Baada ya miaka 5 barabara zitajaa matuta yasiyoweza kuzalisha viazi!

Faida ya kuwa na Miundo mbinu imara ya reli kwa nchi ya Tanzania inayopakana na nchi zaidi ya 8! 6 katika hizo hazipakani na bahari ni mgodi wa kudumu zaidi ya gesi na madini mengine ! Uamuzi wa kuikarabati  reli ya kati itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani 6m kwa mwaka wakati huo huo kurahisisha ujenzi wa reli mpya ya standard gauge! Kimkakati kuna mizigo ya reli na mizigo ya Barabara!  Sasa tear na wares ya malori ni kubwa ni kujaribu kubeba shehena ya reli ! Tokea lini punda akaweza kubeba mzigo wa tembo?  Serikali ya awamu ya 5 inapaswa kuchukua deni kubwa la reli kufanya utaratibu wa kupatikana working capital na ajira mpya baada ya miaka mitano Wanareli  wapya wakabidhiwe reli mpya iendeshwe kwa ufanisi na itoe tija ! Kupuuza kumpa yule Ng'ombe lishe halisi na kutarajia maziwa mengi kwa maana ya  huduma ya  kisasa ni ndoto ya Alinacha!  

Naamini pale TRL hata wakija  Malaika kuongoza bila mtaji wa kazi ( Working Capital) na ajira mpya na ukarabati wa reli ya kati huduma ya reli haitopata tija!  Mungu Ibariki Huduma ya Reli ! Mungu Ibariki Awamu ya 5 ya JM!

No comments