WAZIRI HASUNGA AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA LA KILIMO HAI MJINI DODOMA
 Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akipata maelezo toka kwa Afisa Mshauri wa Mawasiliano wa TOAM, Akitanda Constantine kuhusu mbolea na dawa za asilia ijulikanayo kama slan ya kibailojia alipotembelea banda la kampuni ya Ewen Agri Limited alipotembelea maonesho ya bidhaa za Kilimo Hai jijini Dodoma leo. ngalia boga la asili lililokuwa kwenye manesho ya bidhaa za wakulima kwenye mabanda yaliandaliwa sanjari na Mkutano wa Kitaifa wa Kilimo Hai jijini Dodoma.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Emeci Tchnologies Limited, Deusdedit Kizito akitoa maelezo ya asali mbichi ya asili inavyoandaliwa Waziri huyo alipotembelea banda la kampuni katika maonesho ya bidhaa za Kilimo Hai jijini Dodoma leo. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti Kitaifa EOA, Beatus Malema, Mkurugenzi wa Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) Janet Maro na Mwakilishi Mkazi wa shirika la FAO, Fred Kafeero.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akifurahia mbegu ya mboga aina ya chaya yenye protini nyingi alipotembelea banda la kampuni ya ECHO kwenye maonesho ya bidhaa za Kilimo Hai jijini Dodoma leo. Kulia ni Msaidizi wa Kampuni hiyo, Mary Bonaventure.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akisalimiana na Mwakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa Nchini, Cecile Frobert alipowasili kufungua Mkutano wa Kitaifa wa Kilimo Hai ulioanza leo mjini Dodoma. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO, Fred Kafeero.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akipata maelezo toka kwa Dkt. Never Mwambela, Mtafiti na mgunduzi wa kiuatilifu hai (Biopesticicle) ya vuruga kwa ajili ya kudhibiti viwavijeshi vamizi, kantamze na wadudu wa pamba alipotembelea moja ya banda kwenye maonesho ya bidhaa za Kilimo Hai jijini Dodoma leo.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wa ‘Kilimo Hai’ walishiriki mkutano huo jijini Dodoma leo.  Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali.  Mkurugenzi wa TOAM, Jordan Gama akizungumza machachewakati wa ufunguzi wa Mkutano wakitaifa wa Kilimo Hai jijini Dodoma Novemba 26 2019.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa nne kulia) akipata maelezo ya viungo toka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Zanzibar Spices and Heritage Center, Foum Ali Guru alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya bidhaa za Kilimo Hai jijini Dodoma leo. Kutoka (kulia) ni Mkurugenzi wa Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) Janet Maro, Mwakilishi Mkazi wa shirika la FAO, Fred Kafeero na Mkurugenzi wa TOAM, Jordan Gama  Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakiembelea mabadanda na kujionea mbegu na bidhaa za ‘Kilimo Hai’ katika maonesho yaliyondaliwa sanjari na mkutano huo.  Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakiembelea mabadanda na kujionea mbegu na bidhaa za ‘Kilimo Hai’ katika maonesho yaliyondaliwa sanjari na mkutano huo.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akiangalia boga la asili lililokuwa kwenye maonesho ya bidhaa za wakulima kwenye mabanda yaliandaliwa sanjari na mkutano wa Kitaifa wa Kilimo Hai jijini Dodoma Novemba 26 2019. Mkutano huo umeandaliwa na Shirika linalojihusha na Kilimo Hai Tanzania (TOAM), FAO na wadau wengine mbalimbali. Kutoka (kushoto) ni Mwakilishi Mkazi wa shirika la FAO, Fred Kafeero, Mwenyekiti Kitaifa wa EOA, Beatus Malema, Mkurugenzi wa TOAM, Jordan Gama na mkulima wa boga hilo, Elibariki Joseph (kulia). (PICHA NA ROBERT OKANDA)
Post a Comment