JPM AONGEZA SIKU 20 ZA USAJILI WA SIMU AHIMIZA ZITUMIKE VIZURI!
Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ameongeza siku 20 zaidi za usajili wa simu kwa alama za vidole 'biometria'. Inatarajiwa Watanzania wote waliokabiliwa na changamoto za aina mbalimbali na kuwazuia kukamilisha usajili wa simu zao kwa wakati wataitumia fursa hii alioitoa Rais leo mjini Chato baada ya yeye mwenyewe kukamilisha usajili wa laini yake kwa kutumia biometria!
Changamoto kubwa ni Watanzania wengi kutokuwa na kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Utoaji ya Vitambulisho vya Taifa-NIDA. Nida hivi karibuni ilitoa tangazo kuwa katika siku 7 za mwisho wa mwezi wa Desemba watafanya kazi usiku na mchana ili kukiidhi mahitaji ya Wananchi wanaohitaji kupatiwa namba za usajili wa vitambulisho vya Taifa.
Ni matarajio yetu kuwa NIDA wataendelea kufanya kwa saa 24 ili siku 20 alizoongeza Ndugu Rais(kuanzia Januari Mosi hadi 20, 2020) zitumike kwa lengo lililokusudiwa kuwahudumia wale Watanzania waliokuwa wamefikwa na dharura wakati wa zoezi likiendelea la usajili laini za zimu kwa biometria lililoanza mapema mwaka huu unaoisha wa 2019.
Post a Comment