BALOZI WA UJERUMANI NCHINI MHE.REGINE HESS ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUJIONEA KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO INAYOFANYWA KWA USHIRIKIANO WA JKCI,ISRAEL NA UJERUMANI
Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess akizungumza na mama wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji mdogo wa moyo wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja wa kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani.
Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess akizungumza na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani alipotembelea JKCI kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo. Katika kambi hiyo watoto 55 walifanyiwa uchunguzi wa moyo, kati ya hao 18 walifanyiwa upasuaji mdogo wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba, saba watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi na 30 watatibiwa hapa nchini.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka nchini Ujerumani Felix Berger akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess jinsi tundu la moyo linavyozibwa kwa njia ya upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu kutoka JKCI, Israel na Ujerumani. Kushoto ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka nchini Ujerumani Felix Berger.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess na wataalamu wa afya kutoja JKCI, Ujerumani na Israel mara baada ya balozi huyo kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu kutoka JKCI, Israel na Ujerumani. Katika kambi hiyo watoto 55 walifanyiwa uchunguzi wa moyo, kati ya hao 18 walifanyiwa upasuaji mdogo wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba, saba watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi na 30 watatibiwa hapa nchini.
Post a Comment