HII SIO PICHA YA WUHAN CHINA BALI NI IIGIZO LA KAMBI YA MATESO YA MANAZI YA KATZBACH IKIWA NI KUMBUKUMBU YA KUUAWA WATU 528 MWAKA 1945 !
Hii picha inatumika vibaya katika mitandao kana kwamba ni wahanga wa virusi vya ajabu vya 'corona' huko jijini Wuhan China. Ukweli hiyo picha ni ya Waaigizaji ikiwa ni mradi maalum nchini Ujerumani kuadhimisha mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Majeshi ya Kifashisti ya Manazi wa Kijerumani. Mauaji hayo walifanyiwa Wafungwa waliokuwa wanashikiliwa katika kambi za mateso anuai nchini Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya pili ya Dunia(1939-1945).
Kambi ya Mateso ya Manazi Katzbach ikiwa ni kumbukumbu ya kuuawa watu 528! Wahanga hao walizikwa katika makaburi ya jiji la Frankfurt. Kambi nyingine za mateso walikotoka wahanga ni Buchenwald na Dachau. Msafara huo kuelekea katika mauaji ya kimbari ulifanyika Machi 24, 1945.
Post a Comment