Finlandia kupunguza muda wa kazi !
Bi Sanna Marin Waziri Mkuu Mpya wa Finlandia
Bi Marin amekuja na mtizamo mpya wenye lengo la kuboresha mazingira ya kazi Finlandia! Ikiwa ni kupunguza muda wa kufanya kazi kutoka saa 8 hadi saa 6 na kutoka siku 5 kwa wiki na kuwa siku 4!
Waziri Mkuu mpya wa Finlandia Bi Sanna Marin ametoa wito wa kuanza utaratibu mbadala ambao utaruhusu kufanya kazi kwa saa 6 tu katika siku 4 za kazi kwa wiki.
Sanna Marin, Mwanamke mwenye umri mdogo kwa sasa duniani anayeshika wadhifa wa kuongoza Serikali, ametangaza kusudio hilo lifanyiwe kazi akiamini ni hatua ya maana katika maisha ya kufanya kazi.
Waziri Mkuu huyu kinda mwenye umri wa miaka 34 anaongoza Serikali ya mseto ya Vyama vitano vya siasa vya mrengo wakati na wa kijamaa. Vyama vyote hivyo vinaongozwa na Kinamama.
Waziri Mkuu Sanna Marin
Kiongozi huyo wa Social Democratic Party ameliambia jarida la NewEurope: " Nina amini watu wanapaswa kutumia muda wao mwingi na familia zao, wapenzi wao na kushiriki harakati zingine wazipendazo kimaisha na kijamii ikiwemo shughuli za kitamaduni. Hii itakuwa hatua kubwa ya kuboresha mazingira katika maisha yetu ya kikazi".
Hivi sasa Wafini wanafanya kazi kwa saa 8 kila siku kwa siku tano za wiki.
Kuanzia mwaka 1996 Wafini walikuwa na haki ya kufanya kazi kwa saa 8 au 5 kwa siku ikitegemea mahitaji na utashi wa mfanyakazi.
Aidha jirani zao wa Sweden tokea mwaka 2015 wanatumia huu mtindo mpya wa kufanya kwa saa 6 katika siku 4 za kazi kwa wiki. Utafiti uliofanywa umeonesha huo mtindo umeongezea wafanyakazi furaha ya kijamii aidha kipato chao kimeongezeka sambamba na tija kazini.
Post a Comment