RAIS MAGUFULI AWATAKA VIONGOZI WAPYA ALIOWAAPISHA KUCHAPA KAZI KWA UADILIFU NA KUTANGULIZA MBELE MASLAHI YA TANZANIA
Viongozi waliopishwa wakila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Januari, 2020 amewaapisha Mawaziri 2 na Mabalozi 3 aliowateua hivi Karibuni.Mawaziri walioapishwa ni George Boniface Mwataguluvala Simbachawene aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mussa Azzan Zungu aliyeapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mabalozi walioapishwa ni Mhe. Maimuna Kibenga Tarishi aliyeapishwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva – Uswisi, Hussein Athuman Kattanga aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Tokyo – Japan na Prof. Kennedy Godfrey Gastorn aliyeapishwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa New York Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kuwaapisha na kushuhudia wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Rais Magufuli amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uchapakazi, kutanguliza maslahi ya Tanzania pamoja na kushirikiana vizuri na viongozi na watendaji wengine katika wizara zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Hussein Kattanga kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan
Amemtaka Mhe. Waziri Simbachawene kushughulikia dosari zilizopo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwemo kuhakikisha watendaji na viongozi ambao ni kikwazo katika ufanisi wa wizara wanaondolewa, pamoja na kushughulikia makubaliano yaliyotiwa saini na viongozi wakuu wa wizara waliopita kuhusu mkataba wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto (vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni 1) katika mazingira yasiyokuwa na uadilifu na bila kujali maslahi ya Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Kennedy Gastorn kuwa Balozi wa kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa New York katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene Nyaraka zenye makubaliano (MoU) zilizotiwa saini na Viongozi wakuu wa Wizara hiyo ambao hawapo kwa sasa kuhusu ununuzi wa vifaa mbalimbali vya Jeshi la Zimamoto ili aifanyie kazi haraka.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu akizungumza mara baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Maimuna Tarishi kuwa Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene akizungumza jambo na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu kabla ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam
Post a Comment