JENGENI UTAMADUNI WA KUTEMBELEA VIVUTIO VILIVYOPO-NAIBU WAZIRI SHONZA
Na Vero Ignatus,Manyara
Twiga nao ni baadhi ya wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Tarangire ,wakiwemo Simba,chita,chui,na Chatu,Tai na aina 550 za ndege na vivutio vingine vingi.
Mawaziri pamoja na viongozi kutoka katika nchi wanachama wa Umoja wa Posta Afrika PAPO wametembelea H ifadhi ya Taifa Tarangire ambapo ni makazi ya Tembo wengi kwa eneo la kilometa za mraba kuliko sehemu yeyote duniani
Akizungumza Posta Masta Mkuu Hassan Mwang’ombe amesema kuwa wageni hao wanapokuja kwenye nchi ya Tanzania wanavitu vingi vya kujifunza hivyo wamewaleta katika Hifadhi hiyo ya Tarangire ili kufurahia moja ya vivutio vilivyopo katika hifadhi nchini Tanzania
Mwang’ombe amesema kuwa nchi ya Tanzania ina vivutio vingi vya asili hivyo ujio wa wageni hao ni safari ya kutangaza utalii ndani na katika Mataifa mengine
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Tanzania imekuwa ikitangaza masuala ya utalii hivyo wamewaomba wageni waliofika hifadhini watakaporudi katika nchi zao (ambao ni zaidi ya nchi 40)wakawe mabalozi wazuri katika kuutangaza utalii huo.
Baadhi ya wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Tarangire,Vivutio vingine ni Miti mikubwa ya Mibuyu,uhamaji wa wanyama pori,Mto Tarangire,Mabwawa.
Amesema Wizara ya utalii imekuwa ikihamasisha utalii wa ndani kwamba wananchi wenyewe wajijengee tabia ya au utaratibu wa kutembelea vivutio vilivyoko
Akizungumza na wageni hao kutoka nchi mbalimbali barani Afrika Afisa Mhifadhi Mkuu na mkuu wa kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Utalii Hifadhi ya Tarangire amesema kuwa wengi wa Wanyama wengi hutoka nje ya hifadhi kwenda kwenye maeneo ya ardhi inayozalisha na wengi wao huzaliana huko.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzitembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire pamoja na wageni waliokuja nchini kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU)
Amesema kuwa Zaidi ya aina 550 ya ndege hupatikana katika hifadhi hiyo miongoni mwao wakiwa ni ndege wahamao mabara mengine ambapo savanna ya miombo katika hifadhi hiyo ni moja yenye maeneo ya utajiri mkubwa kwa kuwa ni mazalio ya ndege.
Amesema kuwa Mfumo wa mto Tarangire ni chanzo pekee cha maji cha kuaminika kwa uoto wa asili wa masai stepp nyakati za ukame ambapo ukame kwa kawaida hutokea kati ya julai -novemba kwani mamalia wakubwa waliotawanyika katika nyika hurudi mtoni mara visima vya asili vya nje ya hifadhi vinapokauka.
Afisa Mhifadhi Mkuu na Mkuu wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Tarangire akizungumza na wageni katika eneo la geti la kuingilia.
‘’Muonekano wa mazingira ni rahisi sana kipindi hiki cha mwaka kwani Wanyama wengi hufika mtoni na kingo zake kwaajili ya maji mara moja kwa siku sehemu yam to inaweza kukauka pale maji yanapozama chini ya mchanga ’’alisema.
Katika hifadhi hiyo ya Tarangire mabwawa yaliyoenea katika hifadhi ni vyanzo muhimu vya maji na hutengeneza hifadhi muhimu haswa wakati wa ukame kwaajili ya tembo ambapo mabwawa hayo hupatikana mashariki na kusini mwa hifadhi.
‘’Huingiza maji katika mto unaopeleka maji kaskazini na magharibi na kisha kuishia ziwa Burunge ambalo ni ziwa la msimu ,hifadhi hii muhimu ilianzishwa ili kulinda vyanzo vya maji kwaajili ya viumbe hai’’alisema
Aidha hifadhi ya Taifa ya Tarangire ipo umbali wa kilometa 120 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA)ina ukubwa wa kilometa za mraba 2850 na hivyo kuifanya kuwa hifadhi ya sita kwa ukubwa Tanzania.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiwa na Afisa Mhifadhi Mkuu na Mkuu wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Tarangire
Wageni wakipewa maelezo kabla ya kuingia hifadhini geti la na mmjoja wa kiongozi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire
Sifa mojawapo ya Hifadhi ya Tarangire ni Makao ya tembo wengi kwa eneo la kilometa za mraba kuliko sehemu yeyote nyingime duniani,pia inasemekana kwamba ni mnyama anayeweza kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu.
Post a Comment