RAIS SHEIN ATUNUKU NISHANI IKULU ZANZIBAR
Na Mwandishi Maalum, Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ametunuku Nishani ya Mapinduzi, Nishani ya Utumishi Uliotukuka pamoja na Nishani ya Ushujaa kwa Viongozi, Watumishi wa Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara Maalum za SMZ na wananchi mbali mbali wenye sifa maalum.
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya siasa, viongozi wakuu wastaafu akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk, Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Kwa Viongozi na Wananchi Wenye Sifa Maalum.Ndg. Hassan Juma Khamis, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha, Mawaziri na Viongozi wengine wa Serikali.
Aidha Wanafamilia za Watunukiwa na Wananchi kwa ujumla walikuwemo katika watu waliohudhuria hafla hii ambayo ni muendelelezo wa shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi Wenye Sifa Maalum.Bi. Khadija Hassan Aboud, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Mapema akitoa tamko la Kwanza la kuashiria kuanza shughuli hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum alisema kuwa Rais Dk. Shein ametunuku Nishani 37 ya Mapinduzi, Nishani 10 ya Utumishi Uliotukuka na Nishani 25 ya Ushujaa kwa Viongozi, Watumishi wa Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara Maalum za SMZ pamoja na wananchi mbali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi Wenye Sifa Maalum Ndg. Haji Nassib Haji (Nyanya) hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa sherehe hiyo ilihudhuriwa na watunukiwa 72 ambao kati ya hao 22 ni Marehemu ambao Nishani zao zimepokelewa na wawakilishi wao na 50 wako hai ambapo nishani zao watapokea wenyewe au zitapokewa kwa niaba yao.
Alisema kuwa Watunuku wote sifa zao zimekidhi matakwa ya Nishani hizo ambapo Nishani ya Mapinduzi hutolewa kwa mtu ambaye aliasisi au alishiriki au aliyatukuza na aliyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.
Post a Comment