Ads

MELI KUBWA YA UTALII ILIYOBEBA WATALII 600 YAFUNGA GATI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO!

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Malengo ya Tanzania kufikisha Watalii Milioni mbili kwa mwaka yameanza kutimia, baada ya Watalii  zaidi ya 600 kutoka mataifa mbalimbali duniani kuwasili nchini kwa ajili ya ya kufanya utalii katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi (Januari 9, 2020) Kaimu Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Joseph Sendwa alisema ujio wa watalii hao utaongeza chachu ya Mapato na kuufanya uchumi wa nchi kuinuka kupitia sekta ya Utalii.



Watalii wakishuka

“Ujio wa Meli ya Watalii hapa nchini pamoja na Watalii kutembea  katika Jiji letu la Dar es Salaam, watatumia magari hivyo mzunguko wa mapato utakuwa mkubwa ukiachilia mbali na mapato ya uhamiaji pindi wageni wanakiwasili nchini” alisema Sendwa. Aidha Sendwa alisema TTB itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza sekta ya utalii nchini ambapo imedhamiria kuweka mazingira rafiki katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha kuwa gati na.  1, 2, 4, 5 na 7 katika Bandari ya Dar es Salaam zinapokea idadi kubwa ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.“Meli hii ya watalii imetia nanga hapa kwenye Gati jipya kabisa, kwetu sisi ni fahari na tunajivunia sana kwa hili, hivyo mataraijio yetu hapo baadaye zije meli kama hizi mbili kwa pamoja ili kuongeza mapato katika nchi yetu” alisema Sendwa



Watalii wakishuka

Kwa upande wake Mtalii, Whori Warabisako nchini Japani amesema kuja kwake Tanzania ni fursa moja wapo ya yeye kujifunza utamaduni wa Matanzania na kujione mazingira tulivu yaliyopo hapa nchini“nafurahi kuwepo hapa Tanzania, hii ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania na  nina amini kufika Tanzania nitajifunza mengi katika kuutembelea maneo ya kitalii ya Tanzania” alisema whori Warabisako.



Meli iliyobeba watalii

Watalii hao kutoka Japani, Marekani, China, Tawain, Uingereza wamewasili leo Alhamisi Januari 9, 2020 saa 12 asubuhi wakiwa katika Meli kubwa ya Kisasa ya kampuni AZAMARA  inayofanya safari zake Dunia nzima katika kutangaza utalii wa majini.Meli hiyo ya AZAMARA itaondoka leo Alhamisi Januari 9, 2020 saa 4 usiku kuelekea Zanzibar kwa lengo la kufanya utalii wa ndani katika maeneo ya kihistoria ikiwemo Mji MKongwe Unguja.


No comments