Kasongo Mtendaji Mpya Bodi ya Ligi
Na ALLY SHATRY, Dar
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Almasi Kasongo kuwa Mtendaji mkuu (CEO) mpya wa Bodi ya ligi ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Boniface Wambura aliyemaliza muda wake.
Kasongo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ametangazwa mbele ya Waandishi wa Habari na Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao.
Baada ya kutangazwa Kasongo ameushukuru uongozi wa TFF kwa kumuamini na kuahidi kufanya kazi kwa uadilifu licha ya kuwa na changamoto nyingi.
“Nawashukuru sana TFF kwa kuniamini ma kunipa nafasi hii na kipaumbele changu cha kwanza kitakuwa na leseni za klabu (club lisence) uzalishaji mapato, uendeshaji wa mahusiano kwa umma,” alisema Kasongo.
Post a Comment