Ads

YALIOTOKANA NA KIKAO CHA KUJADILI MAUDHUI KATIKA TASNIA YA HABARI!

Kikao hapa ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam cha kujadili Kanuni za kuratibu Maudhui katika vyombo vya habari vya kawaida na mitandao ya jamii kimemalizika na kufungwa rasmi na Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo(WHUSM) Profesa Elisante Ole'Gabriel saa 7:47 mchana.

Profesa ameahidi michango yote itazingatiwa ikiwemo na ile ya maandishi kutoka kwa Wadau wote ambao kwa wale waliobado kuwasilisha, siku ya mwisho kufanya hivyo ni siku ya  Ijumaa ijayo Oktoba 06, 2017!

Hata hivyo 'Maez Habari Blog'  ilivutiwa na mchango wa Kiongozi wa East Africa Radio Nd Nasser Kingu. Ambaye katika mchango wake mubashara alitahadharisha kuwa baadhi ya mapendekezo ya kanuni yataathiri Radio ambazo husajiliwa kupiga muziki maalum(jazz, reggae au charanga) kwa  vile kanuni zinataka muziki wenye asili ya Tanzania uchezwe kwa asilimia 85! 

Alisisitiza kanuni za sasa zinazotaka asilimi 60 za muziki wa Tanzania inatosha!
Katibu Mkuu wa WHUSM aliahidi kuzingatia matakwa ya walaji ambayo yanatambuliwa rasmi.

No comments