MAKAMU WA RAIS SAMIA NA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE WAUNGANA NA WADAU KUCHANGIA HARAMBEE YA UJENZI WA UKUMBI WA CCM PWANI
Na Mwandishi Maalum, Kibaha
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana kwa Ishara na Viongozi wa Mkoa wa Pwani alipowasili katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Pwani Machi 14, 2020 kwa ajili ya kuongoza Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani. Jumla ya Shilingi Milioni zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo.
Makamu wa Rais na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu pamoja na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wameungana na wadau , kwenye harambee ya kuchangia zaidi ya TZS milioni 500 ili kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa CCM mkoani Pwani, ":ambapo ameeleza chama hicho mkoa sio maskini badala yake waviendeleze vitega uchumi walivyonavyo.
Katika harambee hiyo, imeweza kupatikana kiasi cha TZS milioni 584.1 ikiwa fedha taslim TZS milioni 113.4,ahadi TZS milioni 471.6, mifuko ya saruji 400 na ndoo za rangi 50.
Akizungumza katika harambee hiyo iliyofanyika mjini Kibaha, Samia alisema ofisi yake inachangia TZS milioni kumi na kudai ,jengo hilo lilisuasua kwa kipindi kirefu lakini chini ya usimamizi wake atasimamia ujenzi huo na hakuna fedha wala nondo zitakazopotea kama zilivyopotea wakati huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno akimkabidhi Tuzo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi la CCM Mkoa wa Pwani uliofanyika Machi 14, 2020 Kibaha Mjini.
Alisema, CCM Pwani ina vitega uchumi ,lakini waache kubakia kuvihesabu kwa namba ,wasilale badala yake waviendeleze ili kupiga hatua kiuchumi na kuondokana na hali ya kuwa omba omba.
"Sisi sio masikini wa namna hiyo, tuliendekeza matumbo kuliko lililo mbele yetu, sasa tuache kuendekeza matumbo tufanye kazi,mkoa wa Pwani hauna sababu ya kupita kuombaomba, maana mna mtaji lakini pia mmelala."
"Tujipange vizuri, itabakia tunasema hiki chetu, kile chetu lakini hamviendelezi". Alibainisha Samia.
Samia alifafanua, wahakikishe jengo hilo linakamilika mwezi June mwaka huu ili kuondokana na kupanga ukumbi wakati wa shughuli za Chama.
Nae , Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alishukuru na kufurahi kwa kualikwa kwenye shughuli hiyo,na atachangia mifuko 200 ya saruji.
Jakaya alisema ,wazo la ujenzi huo lina historia kwake, lilianza miaka mingi ,":Nimefurahi sana kuona msukumo wa kuendeleza vitega uchumi hivi ambavyo vilisuasua lakini sasa vinaendelezwa kwa manufaa ya chama." Alisema Rais huyo Mstaafu.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,aliwaomba ,Wadau na Wananchi kuendelea kuchangia ili kutimiza adhma hiyo.
"Tumepewa muda ,hadi mwezi June mwaka huu ,ujenzi uwe umekamilika hivyo juhudi za pamoja zinatakiwa ili tukamilishe kwa wakati huo". Alifafanua Ndikilo.
Katika harambee hiyo, Mfanyabiashara Bakhresa amechangia kiasi cha TZS milioni 100 wakati Subash Patel anaezeka jengo zima kwa gharama ya TZS 250.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndikilo alitoa TZS milioni 50, kamati ya siasa mkoa mifuko 200 ya saruji na TZS milioni nne,Wabunge 13 wa mkoa huo wamechangia TZS milioni 16, ambapo rafiki wa Mbunge wa Viti Maalum Zainab Vullu amechangia TZS milioni 10.
Mhandisi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani Suleiman Nassor akimuelezea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhusu Jengo hilo litakavyokuwa wakati Makamu wa Rais alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo Machi 14, 2020 Kibaha Mjini.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza Jambo kwa Viongozi wa Mkoa wa Pwani kuhusu Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo Kibaha Mjini Machi 14, 2020. Kulia ni Rais Mstaafu awamu ya Nne Mhe. Jakaya Kikwete.
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Ali Makoa akimuelezea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhusu litakavyokuwa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani litakapokamilika alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo Machi 14, 2020 Kibaha Mjini.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi, Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani iliyofanyika Machi 14, 2020 katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Mjini. Jumla ya shilingi Milioni zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza Jambo kwa Viongozi wa Mkoa wa Pwani kuhusu Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo Kibaha Mjini Machi 14, 2020.kulia ni Rais Mstaafu awamu ya Nne Mhe. Jakaya Kikwete.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Kikwete akizungumza kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani iliyoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Mjini March 2020.
Jengo la Ofisi na ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani. Jumla ya Shilingi Milioni zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo.
(Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Post a Comment