Ads

WATOA HUDUMA WA FEDHA KUANZA KUSAJILIWA MWEZI HUU,WAMO MAWAKALA WA PESA KWA NJIA YA SIMU YA MKONONI




Na Mwandishi Maalum, Arusha





Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bw.Bernard Dadi akizungumza kwenye Semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha inayoendelea jijini Arusha, kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha,na ufafanuzi zaidi kuhusu

kusajiliwa kwa Watoa huduma wa Fedha nchini.

Dadi amesema kuwa usajili huo utakuwa ni wa lazima kwa yoyote atakaye husika na utoaji wa huduma wa Fedha,na kwamba usajili huo unatarajiwa kuanza rasmi Mwezi Machi-Aprili 2020 kwa awamu ya kwanza,na awamu ya pili utaanza Mwezi Mei mpaka Juni mwaka huu.

Akifafanua zaidi kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha  (Financial Services Registry) ,Dadi alisema watoa huduma wa Fedha wote wakiwemo mawakala wa Pesa kwa njia ya simu ya mkononi ni lazima wasajiliwe.

“Kila mtoa huduma wa fedha lazima ajisajili, vinginevyo hataweza kuendelea kutoa huduma hiyo kwa vile mfumo hautamtambua.” Alisisitiza.

Akieleza sababu za kuanzishwa kwa mfumo huo Bw. Dadi alisema, kukidhi matakwa ya sheria ya Mifumo ya malipo ya Taifa (NPS Act ya 2015), upatikanaji wa taarifa zinazoendana na wakati na timilifu, upimaji wa viashiria vya Mpango Mkakati wa huduma jumuishi za kifedha (NFIF), kuwezesha maamuzi ya kibiashara na mipango mkakati na kusaidia utambuzi wa maeneo yenye ukosefu wa huduma.

“Ili mtu aweze kusajiliwa lazima awe na kitambulisho kimoja kati ya vitambulisho vitano vinavyotambuliwa na Benki Kuu ambavyo ni Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha kupigia kura au Pasi ya Kusafiria.” Alibainisha.

 Alisema Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekasimu shughuli hizo za usajili kwenye Halmashauri mbalimbali kote nchini na kwamba mawakala wadogo wa kundi la nne ambao ndio wengi wasiwe na wasiwasi kwani huduma hizo zitatolewa kwenye ngazi ya serikali za Mitaa chini ya Taasisi ya Financial Sector Development Trust (FSDT).




Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Bernard Dadi akiwasilisha mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha_(Financial Services Registry) katika semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha.


Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Bernard Dadi akijibu moja ya swali kutoka kwa Mwanahabari (hayupo pichani) kuhusu taratibu za kusajiliwa ikiwa mtu atahitaji kutoa huduma ya fedha,wakati akiwasilisha mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha_(Financial Services Registry) katika semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha.



Meneja wa Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Zalia Mbeo, akifafanua jambo kwenye Semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha,Lengo ya semina hiyo ikiwa ni kuwajengea Uwezo wanahabari hao katika masuala mbali mbali ya Fedha,Uchumi na Biashara.



Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina akizungumza jambo wakati wa semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha inayofanyika jijini Arusha,kwa lengo la kuwajengea uwezo.



Mmoja wa Wanahabari akiuliza swali



Baadhi ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha wakifuatilia mada iliyohusu mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha na umuhimu wake kwa watoa huduma za fedha


No comments