Haya ni mahojiano ya Mwandishi Charles Mulinda na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulid Banyani kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo katika kipindi cha takriban miaka mitano sasa ya Serikali ya Awamu ya Tano. Ofisi za Shirika hili kongwe zipo Barabara ya Ufukoni, Upanga Jijini Dar es Salaam. Mahojiano haya yametoa fursa ya kupata ufafanuzi wa mambo kadha wa kadha yahusuyo utekelezaji wa majukumu ya Shirika kwa Miaka mitano iliyopita.
SWALI: Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Nyumba la Taifa ni moja ya mashirika muhimu sana katika ustawi wa jamii likiwa na jukumu la kuwapatia wananchi makazi bora. Je, ni kwa kiwango gani NHC limefanikiwa kutekeleza jukumu lake hilo la kuwapatia Watanzania makazi bora ndani ya kipindi cha takriban miaka mitano ya serikali ya Awamu ya Tano kwa kuzingatia ahadi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM?
DK BANYANI: Sina shaka hata kidogo kuwa sisi NHC tuna kila sababu ya kutembea vifua mbele. Tunakwenda mchakamchaka, kazi ya kuwapatia Watanzania makazi bora tunaitekeleza kikamilifu na niseme pia historia ya kuanzishwa kwa Shirika hili
tumeilinda na ndoto za Mwalimu Julius Nyerere ambazo Rais John Pombe Magufuli ameapa kuzitekeleza kwa vitendo
tumefanikiwa sana.
'Nitangulie kuwapa watanzania historia fupi ya NHC ili katika maelezo yangu huko mbele
waelewe vizuri. Shirika la Nyumba la Taifa lilianzishwa mwaka 1962, kwa Sheria ya
Bunge namba 45, lengo likiwa ni kuwapatia wananchi makazi bora.
'Hili ndilo Shirika la kwanza kuanzishwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa nchi yetu na hii ni kwa sababu Mwalimualiamini kuwa malazi bora ni moja ya vitu vitatu muhimu katika maisha ya mwanadamu.
Vitu vingine muhimu ambavyo Mwalimu aliamini ni muhimu katika maisha ya mwanadamu ni chakula na mavazi.
'Kwa hiyo hili ni shirika muhimu sana na lina dhamana kubwa katika ustawi wa jamii yetu.
'Sasa tangu kuanzishwa kwa NHC, limekuwa katika safari ndefu ya kuleta mageuzi kwenye
sekta ya nyumba.
'Katika kipindi cha miaka minne na nusu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Shirika hili limeendelea kutekeleza majukumu yake ya
ujenzi wa nyumba za kuuza na
kupangisha, usimamizi wa nyumba na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali na taasisi zingine kama mkandarasi.
'Sasa ngoja nikwambie kidogo kuhusu juhudi tulizofanya katika kujibu matarajiyo ya Watanzania. Katika eneo la ujenzi wa nyumba, Serikali ya Awamu ya Tano
inapoelekea kutimiza takriban miaka mitano madarakani ya utekelezaji wa Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi (2015/16 hadi 2019/2020), shirika limetekeleza jumla ya miradi 94 ya nyumba za makazi na biashara na kati ya
hiyo, iliyokamilika ni miradi 53.
'Kwenye miradi hii iliyokamilika, zaidi ya nyumba 1100 za gharama nafuu zimejengwa
katika Halmashauri za Wilaya mbalimbali na zaidi ya nyumba 6100 zimejengwa kwa watu
wa kipato cha kati kwa ajili ya makazi na biashara.
'Aidha, Shirika lilianzisha na linaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miji ya pembezoni,
ikiwemo Kawe wenye ukubwa wa ekari 267 na Burka Materves Arusha wenye ukubwa wa ekari 579. Miji hii ya pembezoni inalenga kupunguza msongamano katikati ya miji yetu kwa kuwa inakusudiwa kuwa na mahitaji yote muhimu.
'Ujenzi wa miradi hii mikubwa na midogo unalenga kuchangia utatuzi wa tatizo la uhaba wa nyumba nchini unaokadiriwa kufikia nyumba 3,000,000 pamoja na kukuza mchango wa sekta hii kwenye pato la Taifa.
'Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 iliyonadiwa na Rais John Pombe Magufuli inalitaka shirika kujenga nyumba ili kuwapatia
wananchi makazi bora na nafuu.
'Katika utekelezaji wa Ilani, kwetu sisi NHC dhamira yetu ni kuwa na kasi kubwa ya ujenzi wa nyumba. Katika kipindi hiki cha miaka minne na nusu, niseme sasa wananchi wameweza kununua nyumba tulizojenga
kupitia mikopo ya benki washirika ambazo tuna makubaliano nazo.
'Benki hizi ni pamoja na Benki ya Azania, Bank of Africa, Benki ya CRDB, Benki ya Exim, Benki ya KCB, Benki ya NBC, Benki ya DCB, Commercial Bank of Africa, Benki ya NMB, Banc ABC, NIC na Benki ya Stanbic.
'Nyingine ni First National Bank (FNB), International Commercial Bank (ICB) na Diamond Trust Bank (DTB).
'Kupitia mpango huu, wananchi wengi wamepata fursa ya kumiliki nyumba zao bora na niseme wazi, wananchi wengi
wanaupongeza mpango huu wa Shirika na wenyewe wanasema kwao ni ukombozi mkubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulid Banyani
SWALI: Shirika hili NHC unaloliongoza lina mchango wowote katika kuiwezesha safari ya Serikali kuhamia Dodoma kuwa ya ufanisi?
DK. BANYANI: Tena mkubwa sana. Sera yetu ni kuwa bega kwa bega katika kutimiza malengo ya serikali. Iko hivi, tangu mwanzo kabisa NHC tumekuwa pamoja na serikali
katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
'Miradi hiyo ilitekelezwa
na Shirika kama mkandarasi. Na katika kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma, Shirika lilishiriki kujenga majengo ya Ofisi za Wizara nne eneo la
Mtumba Dodoma uliko mji wa serikali.
'Wizara hizo ni ya Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi, Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara na Wizara ya Nishati.
'Mpaka hapo nadhani umeona jinsi tunavyoshiriki na tunavyoendelea kushiriki
katika safari ya serikali kuhamia Makao Makuu ya nchi Jijini Dodoma.' Kadhalika, pale
Iyumbu Dodoma tumejenga takriban nyumba 300 kwa ajili ya makazi na zimeshauzwa kwa
wananchi na taasisi za serikali.
Jengo la Makao Makuu ya Ewura linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
SWALI: Inavyoonekana NHC ni kama vile limejikita zaidi kwenye nyumba za makazi ya watu na biashara na kwa kiasi fulani, kidogo kwenye miradi ya ujenzi wa majengo ya serikali. Je, kuna mikakati gani ambayo shirika lako linayo au limekwishakuwa nayo ya kusaidia kuondoa tatizo la ofisi kwa taasisi za serikali, nikirejea kwenye safari ya serikali kuhamia Dodoma ambako Wizara nyingi na taasisi za serikali hazikuwa na majengo ya kutosha, achilia mbali miradi hiyo uliyoitaja kuwa imetekelezwa na NHC mkoani Dodoma?
DK BANYANI: 'Hapo naona nirejee kueleza vizuri ili nieleweke. Nimekwishasema kama umenipata vizuri NHC tunakimbizana na serikali mgongoni katika kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu.
'Sisi NHC tunakimbia mchaka mchaka nchi nzima. Ngoja nikwambie, Shirika katika
kuondoa tatizo la makazi na ofisi za watumishi wa umma katika taasisi mbalimbali, limesanifu na kujenga majengo 44 ya Wakala wa Misitu Tanzania ili
kuwapatia makazi na ofisi za kulinda misitu yetu. Aidha, Shirika limekarabati shule kongwe mbalimbali nchini, chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
'Na si hayo tu, Shirika pia limeshiriki katika kujenga nyumba za wafanyakazi katika
Halmashauri za Busokelo iliyoko mkoani Mbeya, Mlele mkoani Katavi, Momba mkoani Songwe, Muheza mkoani Tanga na Chato
mkoani Geita.
'Kote huko NHC limekanyanga na limeacha alama ya utendaji kazi wa kupigiwa mfano wa Serikali ya Awamu ya Tano.
'Lakini pia ili kufanya Halmashauri za Wilaya kuwa na majengo ya kisasa ya Ofisi na
kuongeza tija, Shirika la Nyumba la Taifa limejenga majengo ya ofisi katika Halmashauri ya Malinyi na Halmashauri ya
Wanging’ombe na pia Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya ya Hai na Malinyi.
'Mlolongo wa miradi inayotekelezwa na NHC katika serikali ya Awamu ya Tano ni mrefu.Miradi mingine iliyotekelezwa na NHC kwa
ukandarasi katika kipindi hiki ni ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya EWURA Mjini Dodoma na ujenzi wa jengo la Chuo Kikuu
cha Mwalimu Nyerere mkoani Mara.
'Pia tumefanya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Benki la CRDB, Jijini Dar es Salaam, Jengo la Chuo Kikuu cha Ardhi na ujenzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum huko Mbuye Mkoani Geita.
'Kupitia utaratibu huu, Shirika liliaminiwa na serikali na kupewa kujenga miradi ya kimkakati ambayo itaongeza tija kubwa kwa Taifa letu.
'Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa machinjio ya kisasa eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam, ambayo itakuwa na uwezo
wa kuchinja ngombe 1500 na mbuzi 1000 kwa siku, ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya
Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara na Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa, Mjini
Musoma. 'Miradi yote hii inayofanywa na Shirika kama mkandarasi iko 26 na ina
gharama ya shilingi bilioni 86.2 hadi kuikamilisha.
'Nizungumzie pia eneo la usimamizi wa nyumba. Hili ni eneo jingine lililopewa
kipaumbele katika kipindi hiki. Shirika limeendelea kujenga uwezo wake kwa kukusanya kodi na malimbikizo kutoka kwa
wapangaji wake na limepangisha nyumba zake zilizojengwa katika Halmashauri za Wilaya na Miji mbalimbali nchini.
'Kwa sasa matengenezo ya nyumba yanazingatia uwiano wa gharama na matengenezo yenyewe ili kuokoa gharama za matengenezo na muda unaotumika katika kazi hii.
Ndugu yangu nikwambie tu
katika kipindi cha takribani miaka mitano, Shirika limeboresha sera yake ya uwajibikaji kwa jamii ambapo kupitia sera hiyo, Shirika lilichangia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na kuboresha sekta ya elimu.
'NHC kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Wakala wa Utafiti wa Vifaa vya Ujenzi na Majengo (NHBRA) na Wakuu wa Mikoa na Wilaya, liliandaa mpango wa mafunzo kwa vijana yaliyoambatana na kuwapatia mashine za kutengeneza matofali yanayofungamana.
'Chini ya mpango huu, Shirika lilitoa mashine nne kwa kila Halmashauri ya Wilaya na mtaji
kidogo kwa ajili ya kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia miradi ya kutengeneza matofali na kujenga nyumba.
'Mpango huu uliwapatia ajira ya moja kwa moja vijana 6400 kwa awamu ya kwanza.
'Sasa Shirika linaendelea na utekelezaji wa majukumu yake ya msingi. Kazi zinazoendelea kufanyika kwa sasa ni pamoja
na kuanza usanifu na maandalizi ya ujenzi wa nyumba 1000 za makazi jijini Dodoma na
tunaendelea na kazi ya ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Kanda ya Kati Dodoma.
'Aidha, Shirika tumeanza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya ujenzi kama vile kokoto, matofali na mabati. Hapa NHC tunatekeleza kwa vitendo ile dhana ya Tanzania ya viwanda.
Ndugu Mwandishi, ukamilishaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba unaendelea na utakamilika katika muda mfupi ujao.
'Kwa kifupi nikuambie tu kuwa katika utekelezaji wa dira ya Serikali ya Awamu ya Tano, Shirika limelenga kuongeza ajira kwa watanzania, kuwapatia makazi bora na kuunga mkono serikali katika ujenzi wa miradi ya kimkakati yenye kuboresha maisha ya watanzania.
'Nisema tu kwamba sekta ya nyumba ni sekta mtambuka kwa kuwa huchochea ukuaji wa
uchumi na kukuza uwekezaji. Aidha, sekta hii ni moja ya sekta zinazoongoza kwa kuwapatia wananchi ajira.
'Sekta hii ina wajenzi, mama na baba lishe, wauzaji wa vifaa vya ujenzi wote ajira zao ni za uhakika kama sekta ya nyumba inakuwa endelevu. Kwa kuzingatia mchango wa sekta
ya nyumba tutaendelea kufanya kazi kwa bidi ili iwe chachu ya maendeleo ya Tifa letu.
Nadhani nimeeleza kwa vya kutosha ingawa najua bado yapo mengi ya kuwafahamisha
Watanzania kuhusu NHC.
'Hili nitalitelekeza mapema iwezekanavyo. Watanzania wana haki ya kujua Shirika lao la
Nyumba linafanya nini na je linaendana na kasi ya ujenzi wa Tanzania mpya ya Rais
John Pombe Magufuli? Mimi nawaambia NHC tunakimbia sambamba na Rais John
Post a Comment