Ads

KAWOGO ATIA NIA KUGOMBEA JIMBO LA BAGAMOYO!



LEO HII
Mimi Albert Kawogo Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Bagamoyo, Mwenyekiti Taifa wa  Friends of CCM Media Network, Mwanahabari mkongwe, Mkurugenzi wa Kampuni ya INDEPENDENT VOICE LIMITED na mmiliki wa gazeti la SAUTI HURU ni rasmi sasa NIMETANGAZA azma yangu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bagamoyo kupitia CHAMA CHA MAPINDUZI CCM. Demokrasia kwa chama chochote makini cha siasa hukamilika wakati wa uchaguzi,huu ni muda muafaka sasa wa matumizi ya haki hii nami kwa kushauriana na familia yangu nimeona ni wakati muafaka wa mimi kutumia haki yangu ya kikatiba kuingia katika mbio za Ubunge ili kukamilisha haja na stahiki za kiraia zilizoainishwa katika katiba  tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Naingia Bagamoyo kwa jambo moja kubwa KUWA KIUNGO KATI YA FURSA ZILIZOPO BAGAMOYO NA WANANCHI. Bagamoyo ni TAJIRI kwa muda mrefu sasa imekosa mtu sahihi wa kuunganisha fursa zilizopo na wakazi wake. Kazi kubwa imeshafanywa na Rais wetu Dk John Pombe MAGUFULI kilichobaki sisi ni hamasa tu kwa wananchi,vita kubwa ya Bagamoyo ni  kuamsha ukombozi wa fikra ili ziende sambamba na mabadiliko ya karne ya sasa.
Upande wa pili ni kuwa nakwenda Bungeni kuwasemea Wana-Bagamoyo lakini pia kulinda HADHI ya serikali ya Chama changu,huo ndio wajibu wa kwanza wa Mbunge wa CCM. Wajibu huu haungoji maelekezo ya vikao vya caucus vitukumbushe.In Shaa Allah -Mungu anisaidie!


No comments